title : RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI
kiungo : RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI
RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI
Kampuni ya SGA Security imeadhimisha miaka 33 tangu ianze shughuli zake nchini Tanzania huku ikiwatunuku wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa muda mrefu na kupongezwa na Jeshi la Polisi kwa hatua hii. Shughuli ya kuwatambua wafanyakazi hawa ilihudhuriwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Jumanne Muliro katika ofisi za SGA Masaki ikiwa ni moja ya majukumu yake kuhakikisha makampuni
binafsi ya ulinzi na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa.
binafsi ya ulinzi na usalama yanaendeshwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Kampuni hiyi iliunda kikundi maalumu kijulikanacho kama ‘Club 20’ ambacho kinajumuisha wafanyakazi walioitumikia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20. Kwa sasa kampuni ya SGA Security imeajiri wafanyakazi zaidi ya 5,100 Tanzania na kuifanya iwe moja ya makampuni makubwa ya usalama nchini. SACP Muliro aliipongeza SGA kwa kujali masilahi ya wafanyakazi na kuongoza kwa mfano huku akisisitiza kuwa makampuni mengi ya ulinzi na usalama hayafuati utaratibu uliowekwa ikiwemo mafunzo, usimamizi na mishahara huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa SGA.
Mgeni rasmi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Jumanne Muliro akizungumza jambo kabla ya kukabidhi tuzo kwa wafanyakazi wa kampuni ya SGA katika kuadhimisha miaka 33 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya ofisi za SGA.
“Ni jambo la kupongezwa sana kwa kuwa kampuni yenye wafanyakazi zaidi ya 50 walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20,” alisema. Alisema SGA ndio ilikuwa kampuni ya kwanza ya binafsi ya ulinzi na usalama kuanziswa Tanzania na imedhihirisha kuwa kuwajali wafanyakazi ndio chanzo cha mafanikio.
“Nimefahaishwa kuwa wafanyakazi walioitumikia SGA kwa zaidi ya miaka kumi ni zaidi ya 1,500 jambo ambalo linastahili pongezi,” alisema huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na makampuni binafsi ya ulinzi na usalama kuhakikisha mkoa unakuwa salama na kuongeza kuwa walinzi wanafanya kazi kubwa katika kuzuia ujambazi.
Naye Mtendaji Mkuu wa SGA Group, Jules Delahaije aliupongeza uongozi wa SGA nchini kwa kuhakikisha wafanyakazi wanaitumikia kampuni kwa muda mrefu na pia kwa kuwatambua na kuwatunuku waliofanya kazi muda mrefu. Aliwapa wafanyakazi hao ngao maalumu za kuonesha utumishi wao kwa zaidi ya mika 20.
“Tukiwa na wafanyakazi zaidi ya 18,000 duniani kubwa kwetu ni watu. Tumewekeza sana katika mafunzo na pia tumehakikisha tunawalipa wafanyakazi wetu vizuri kabisa ikilinganishwa na makampuni mengine ili tuwajengee mazingira bora ya kazi na pia tuwe nao kwa muda mrefu,” alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa SGA Group, Bw. Jules Delahaije akizungumza jambo wakati wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa kuadhimisha miaka 33 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo ambapo RPC wa Kinondoni, Jummane Muliro alikuwa mgeni rasmi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI
yaani makala yote RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/rpc-aipongeza-sga-kwa-weledi-kujali.html
0 Response to "RPC AIPONGEZA SGA KWA WELEDI, KUJALI WAFANYAKAZI"
Post a Comment