title : POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU
kiungo : POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU
POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU
JESHI la polisi mkoani Tanga, limewahadharisha wananchi kuelekea katika msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kama ulipuaji baruti na fataki ikiwemo kuchoma moto matairi barabarani, kwa yeyote atakayefanya hivyo atachukulia hatua za kisheri.
Kamanda mpya wa mkoa huo, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Edward Bukombe, alisema kwamba jeshi hilo linapiga marufuku kwa mtu yeyote kulipua au kusababisha milipuko ikiwemo baruti, fataki na Eksozi za magari, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria namba 13 ya sheria ya milipuko.
“Hivyo wakazi wa mkoa wa Tanga, ni marufuku kuchoma matairi hovyo na kulipua baruti bila kibali, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakae kiuka agizo hili,” alisema RPC Bukombe.
Alisema uzoefu unaonesha kuwa siku za sikukuu watu wengi hujisahau kujiwekea ulinzi ikiwemo kuwaangalia watoto hivyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi kuhakikisha wanachukua hatua za kuwalinda watoto pamoja na nyumba zao ili wahalifu wasitumie mwanya huyo kufanya uhalifu wa kuvunja au watoto kupotea mitaani.
Kamanda Bukombe alisema kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bali aliwakumbusha kuzingatia taratibu za kumbi za burudani kufungwa nyakati za saa 6:00 usiku na hata ibada za mkesha wa Krismasi na Mwaka mpya zimalizike muda huo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo .
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio yaliyotokea kwa kipindi cha mwaka mzima ambapo alisema Jumla ya Silaha 14 za moto zilikamatwa, kushoto ni Afisa Mnadhimu wa Jeshi hilo Mkoani Tanga,Leonce na kulia ni RCO wa mkoa wa Tanga,Justine Masejo(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa
Hivyo makala POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU
yaani makala yote POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/polisi-tanga-yawatahadharisha-wananchi.html
0 Response to "POLISI TANGA YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUELEKEA SIKUKUU"
Post a Comment