NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI

NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI
kiungo : NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI

soma pia


NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI


Na Said Mwishehe,Blogu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa uamuzi wa kuitupa rufaa iliyowasilishwa na mgombea ubunge Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha AFP.

Mgombea huyo alikuwa akipinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomwekea mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Ramadhan Kailima amesema leo jijini Dar es Salaam kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Kailima kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 40(6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ikisomwa pamoja na Kanuni za 34 na 35 za Kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2015, NEC ilipokea rufaa moja kutoka kwa mgombea wa ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

Pia NEC ilipokea rufaa mbili, ya kwanza iliwasilishwa na mgombea wa udiwani Kata Keza – Halmashauri ya Wilaya Ngara kwa tiketi ya CCM akipinga uamuzi wa Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomwekea mgombea wa NCCR - Mageuzi.

Wakati rufaa ya pili ilitoka kwa mgombea wa udiwani Kata ya Kwagunda katika Halmashauri ya Wilaya Korogwe kwa tiketi ya CCM akipinga aumuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo dhidi ya pingamizi alilomuwekea mgombea wa Chama cha Wananchi(CUF.

Kailima amefafanua kwenye kikao chake cha kawaida kilichofanyika Desemba 24, mwaka huu, NEC ilipitia rufaa hizo na kutoa uamuzi. Akizungumzia rufaa ya mgombea ubunge,NEC imekubaliana na uamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi,hivyo mgombea aliyekatiwa rufaa aendelee kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Singida Kaskazini.

Amesema kuhsu rufaa za wagombea udiwani kata ya Keza na Kwagunda, NEC imekubaliana na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi. “Hivyo wagombea udiwani waliokatiwa rufaa waendelee kuwa wagombea wa udiwani katika kata husika,”amsema Kailima.

Ametumia nafasi hiyo kueleza tayari NEC imetuma taarifa ya uamuzi huo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ili watoe taarifa kwa wahusika kuhusu kilichoamriwa.


Hivyo makala NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI

yaani makala yote NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/nec-yambariki-mgombea-ubunge-ccm.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "NEC YAMBARIKI MGOMBEA UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI"

Post a Comment