MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI

MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI
kiungo : MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI

soma pia


MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawakili wapya muda mfupi baada ya kukubaliwa na kusajiliwa. Pichani pia yupo Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma na Majaji.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akizungumza na Mawakili wapya waliokubaliwa na kusajiliwa ambapo katika nasaha zake kwao alisema atawashangaa sana mawakili hao kama watakuwa wazururaji mitaani wakisubiri ajira badala ya kuitumia taaluma yao kujiajiri wenyewe. Hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili hao imefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee
Sehemu ya Mawakili wapya 296 ambao wamekubaliwa na kusajiliwa kuwa Mawakili wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wakashindwa kujizuia kushangilia pale alipowapa changamoto ya kuzitumia fursa zilizopo kujiajiri wenyewe kwa kwenda Mikoani na Wilayani badala ya kung'ang'ania kukaa Dar es Salaam.
Mhe. George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akibadilishana mawazo na Mkurugezi wa Mashtaka ( DPP) Bw. Biswalo Maganga muda mfupi kabla ya hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili 296 wapya katika hafla iliyofanyika leo Ijumaa katika Viwanja vya Karimjee.

Na Mwandhishi maalum.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju, amewataka Mawakili wapya kuzitumia fursa nilizopo kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa. Ametoa ushauri huo leo ( Ijumaa) wakati wa hafla ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya 296. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Karimjee.

“Niwashauri Mawakili wapya, anzeni kufanya kazi. Itashangaza sana, na nitawashangaa sana kama na nyie mtakaa mtaani mkisubiri kuajiriwa badala ya kutumia taaluma na ujuzi milioupata kujiajiri wenyewe” Mhe. Masaju amewataka mawakili hao wa kike na wakiume, na ambao wengi wao ni vijana wa umri wa kati ya miaka 30 na 40, kwenda mikoani na wilayani ambako amesema, kuna fursa nyingi za kujiajiri na pia kuna wateja wengi wenyeuhitaji mkubwa wa kupata huduma ya za kisheria.

“Nendeni mikoani na wilayani badala ya kung’ang’nia kukaa hapa Dar es Salaam na katika majiji na miji mingine mikubwa hapa nchini. Huko mtapata soko kubwa la wananchi wanaohitaji huduma zenu na wenye uwezo wa kulipia huduma hizo kutokana na shughuli zao mbalimbali zikiwamo za kilimo” amesisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kwa wale Mawakili ambao wataajiriwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na katika Utumishi wa Umma. Mwanasheria Mkuu amesema watatakiwa kuzingatia ipasavyo Maadili ya Msingi yanayosimamia utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Hivyo makala MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI

yaani makala yote MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/mwanasheria-mkuu-awataka-mawakili-wapya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWANASHERIA MKUU AWATAKA MAWAKILI WAPYA KUJIARI"

Post a Comment