SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI

SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI
kiungo : SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI

soma pia


SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya  Mkazi Kisutu imeelezwa mkataba uliongiwa na Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando na  Channel 2 Group Corporation (BV1) haukujulikana na bodi ya Wakurugenzi wala bodi ya zabuni za TBC.

Mwanasheria wa  shirika hilo, Gwakisa  Mlawa ameeleza hayo leo Mei mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi alipokuka akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya  Sh.milioni 887. inayomkabili Tido.

Akiongozwa  na Wakili wa Takukuru, Leonard Swai, Gwakisa ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo amedai alifahamu kuwepo kwa mkataba huo baada ya kupelekewa taarifa ya kesi Juni mwaka 2012 na Channel 2 Group Corporation (BV1) ambapo walikuwa wakidai TBC wamekiuka mkataba walioingia kwa ajili ya kuwekeza kwenye mitambo ya digital.

Shahidi huyo alidai, mkataba huo ulisainiwa na Tido na watu wawili wa Channel 2 Group Corporation (BV1)  na kwamba kulikuwepo na nyongeza ya mkataba ama marekebisho ya mkataba yaliyosainiwa Juni, Agosti na Novemba mwaka 2008.

Alidai baada ya kupokea taarifa hiyo, TBC ilimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuomba ushauri na baada ya AG kuliangalia suala hilo Kwa ujumla wake aliagiza ateuliwe mwanasheria wa kimataifa ambaye ni mjuzi katika masuala hayo.

Amedai iliteuliwa kampuni ya uwakili ya Freshfield Bruckhaus Derringer us  LLP ambaye  baada ya kuteuliwa alifika, TBC na kufanya uchunguzi wa nyaraka na kwamba ililipwa maalipo ya awali zaidi ya milioni 800.

Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa kuwa Tido alisababisha hasara kutokana na kiasi hicho cha fedha hicho ambacho kililipwa kwa kampuni hiyo ya uwakili.

Akijibu swali la Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta, kama aliwahi kuiona hiyo mikataba iliyoingiwa na Tido na kwamba ilikuwa ikimpa kazi, channel 2 Group Corporation (BV1) alidai kuwa ilikuwa ni kama wameingia katika makubaliano ya awali ya maandalizi ya mchakato wa kuelekea kwenye digital.

"Wewe kama mwanasheria wa TBC kwa jinsi ulivyoipitia hiyo mikataba ulichukua hatua gani." Aliuliza Maleta, 

Akijibu swali hilo shahidi huyo alidai, taarifa ya kesi ilifika wakati akiwa nje ya TBC lakini baadae alirudi. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kesho

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa Juni 16, mwaka 2008,   akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.


Hivyo makala SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI

yaani makala yote SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/shahidi-adai-mkataba-uliongiwa-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SHAHIDI ADAI MKATABA ULIONGIWA NA MKURUGENZI WA ZAMANI TBC TIDO MHANDO NA BV 1 HAUKUJULIKANA NA BODI YA WAKURUGENZI"

Post a Comment