title : KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA
kiungo : KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA
KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA
Msimamizi wa Kituo cha kurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa cha Namanga mkoani Arusha Ndg. Joseph Nchinga (kushoto) akitoa maelekezo ya mtambo mpya wakurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi (wa kwanza kulia) wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo eneo la Namanga mkoani Arusha leo tarehe 28/12/2017. Kituo hicho kimekamilika na kimeongeza usikivu wa TBC Fm na TBC Taifa kwa umbali wa Kilomita 45 kwa pande zote mbili za mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso (kulia) akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi mtambo mpya wa kurushia matangazo ya TBC Fm na TBC Taifa wakati alipotembelea eneo ambalo mtambo huo umefungwa mtaa wa Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017. Mtambo huo utaongeza usikivu wa TBC Fm na TBC Taifa kwa kanda ya Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi (katikati) akimuelekeza jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Alkan CIT Ngd. Ali Mohamedi (Kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi mpya za Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) zinazojengwa eneo la Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017. Kampuni ya Alkan CIT ndiyo inayojenga ofisi hiyo ambapo ujenzi unatarijiwa kukamilia mwezi Januari 2018. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso.
Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kanda ya Arusha Ndg. Gerald G. Uisso (kushoto) akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan P. Mlawi chumba kitakacho tumika kama studio za TBC FM na TBC Taifa wakati alipo kagau maendeleo ya ujenzi wa ofisi za kanda za shirika hilo zilizoko Njiro jijini Arusha leo tarehe 28/12/2017. Bi Susan ametembelea eneo hilo kukagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa ofisi mpya za TBC kanda ya Arusha, ujenzi huo unatarijiwa kukamilika mwezi januari 2018.
Eneo la ofisi ya Shirika la Utangazaji la Taifa TBC linaloendelea na ujenzi lililopo Njiro mkoani Arusha. Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Susan P. Mlawi alitembelea eneo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi yaliyofikiwa leo Tarehe 28/12/2017.PICHA NA
OCTAVIAN KIMARIO-WHUSM
Hivyo makala KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA
yaani makala yote KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/katibu-mkuu-wizara-ya-habari-atembelea.html
0 Response to "KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI ATEMBELEA TBC-ARUSHA"
Post a Comment