title : DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII.
kiungo : DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII.
DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII.
Mwambawahabari
Na Hamza Temba, Arusha
..............................................................
Wadau wa Utalii Jijini
Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa
kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika
utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza
Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo wakati akichangia
mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa
kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.
Chambulo
alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya
usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja
na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara
wengine matajiri jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki.
“Tunakupongeza
sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae
aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo
mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike
na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.
Awali
akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya
utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo
wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za
Kimarekani 200.
Kwa upande
wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe
Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000,
magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za
Kimarekani 15,000.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).
Kwa upande
wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa
walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000
na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.
Kwa upande
wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la
kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara
ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya
kutekeleza kanuni hizo.
Alisema sehemu
kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo
yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali
wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na
kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.
Katika
hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha
wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake
uanze mapema mwakani, 2018.
Hivyo makala DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII.
yaani makala yote DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/dk-kigwangalla-kilio-chenu-nimekisikia.html
0 Response to "DK KIGWANGALLA - KILIO CHENU NIMEKISIKIA MIMI MWENYE MAMLAKA YA KUFANYA MABADILIKO, APONGEZWA NA WADAU WA UTALII."
Post a Comment