SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI

SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI
kiungo : SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI

soma pia


SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI

  Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana akisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya wakati wa ziara yao ya kuhamasisha wakulima umuhimu wa kuongeza tija ya kilimo hicho
  Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ulanga mara baada ya kuwasili kulia kwake ni Mkuu wa wilaya hiyo Ngolo Malinya
 Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya akisistiza jambo
  Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila  akizungumza kuhusu namna walivyojipanga kuhimiza kilimo cha zao la Korosho wilayani humo
 Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake
 Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kushoto  akiagana na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila mara baada ya kumaliza mazungumzo nae
 Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisistiza jambo wakati akitoa elimu kwa wakulima wa zao hilo kwenye kikundi cha  Igombiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro
 Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba  kulia akisisitiza jambo kwa wakulima hao kuhusu magonjwa hatari yanayolishambulia zao hilo wakati wa uzalishaji wake na namna ya kukabiliana nalo
 MKUU wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Ngolo Malinya katika akiwa na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga  (DAS) Abraham Mwaikwila akifuatiwa na  Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba
Afisa Habari wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akionyeshwa kitu na mmoja wa wakulima wa zao la Korosho wa kikundi cha Igombiro wilayani Ulanga mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kuhamasisha umuhimu wa kulimo hicho

Na.Mwandishi Wetu, Ulanga. 
SERIKALI wilayani Ulanga mkoani Morogoro imesifu jitihada kubwa zinazo fanywa na bodi ya Korosho Tanzania kwa kuwatembelea wakulima ili kuwahamasisha umuhimu wa kulima kilimo chenye tija ili kuongeza uzalishaji ikiwa ni mpango wa kuliendeleza zao hilo. 

Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Ulanga (DAS) Abraham Mwaikwila wakati wakati wa ziara ya viongozi wa Bodi ya Korosho iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kilimo hicho kwa wakulima wilayani Ulanga ikiwemo upuliziaji wa dawa ili kuongeza uzalishaji. 

Viongozi wa bodi ya Korosho ambao walikuwa kwenye ziara hiyo ya uhama sishaji huo ni Afisa Habari wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana na Afisa Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba ambao walikutana na wakulima wanaolima korosho wa kikundi cha Igombiro 

Alisema kwamba wilaya hiyo tokea miaka ya nyuma walikuwa wanalima korosho lakini baadae waliliacha kutokana na kutokuwa na soko la uhakika lakini kwa sasa ili kuhakikisha zao hilo linalimwa kwa tija mwaka jana walipewa ruzuku ya uzalishaji wa miche ya korosho laki tatu ambayo waliigawa kwa wakulima. 

“Sio hilo mikorosho ya zamani iliyokuwepo tulikuwa na Mkurugenzi aliyekuwa akiitwa Isabela Chiluba aliyetoka Tandahimba kwani baada ya kufika aliweza kuja na mwamko mzuri wa kufufua mikorosho ya zamani kwa mfano mwaka jana walipata pembejo na kupulizia mikorosho ya zamani jambo ambalo limefungua ukurasa mpya kwetu “Alisema. 

Alisema kutokana na hilo mwaka huu wanatarajia kuzalisha miche kwa wingi hivyo anaamini bodi ya korosho itakuwa na uhamasishaji mzuri na miche laki tatu iliyotolewa kwa hiyo mwaka huu itakuwa chachu ya wananchi kuhitaji miche utakuwa mkubwa sana. 

Hata hivyo aliiomba bodi ya Korosho kuweka utaratibu wa kuwapa miche ya korosho kutokana na kwamba asilimia kubwa ya mapato kwenye Halamshauri ya Ulanga yanatokana na mazao hivyo anaamini Mkurugezi na timu yake ya idara ya kilimo watajipanga kuhakikisha wanaenda kununua mbegu kwenye vituo vya naindelee ili waweze kupata miche iliyobora na kuwawezesha kuongeza uzalishaji wenye tija. 

Naye kwa upande wake, Mratibu wa zao la Korosho wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro Samweli Masaro alisema kutokana na kuwepo kwa uhamaishaji huo umewawezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 80. 

Ambapo awali ulikuwa kwa kiwango cha chini hali iliyowa ikiwalazimu kutilia mkazo uzalishaji wa zao hilo kwa kuhamasishaji wakulima kulima ikiwemo kutunza miti yao na kupiga dawa jambo ambalo kwa asilimia kubwa limesaidia kuweza kuwawezesha kupata tani hizo ambazo pia wanatarajia huenda zikaongezeka 



Hivyo makala SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI

yaani makala yote SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/serikali-wilayani-ulanga-yasifu-juhudi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI WILAYANI ULANGA YASIFU JUHUDI ZINAZOFANYWA NA BODI YA KOROSHO NCHINI"

Post a Comment