title : ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017
kiungo : ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017
ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Jamii ya wazanzibari imeshauriwa kufikiria mikakati na huduma bora zitakazosaidia kupunguza idadi ya kuzaliwa na kufariki watoto njiti ili ambao wanakuwa mzigo kwao na Serikali kwa jumla.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Ali Abdalla alipokuwa akitoa tamko kwa waandishi wa habari kuhusu siku ya maadhimisho ya watoto njiti duniani katika ukumbi wa Wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Alisema sababu ya kufanyika maadhimisho ya watoto njiti duniani sio kuwabeza watoto hao lakini ni kuamsha hisia na kuinua uwelewa kwa wananchi na watoa huduma ya afya ya watoto hao kwani iwapo hatua zinazofaa hazitachukuliwa wataendelea kuzaliwa na kufariki kwa idadi kubwa.
Alisisitiza kuwa Shirika la Afya duniani linaamini kuwa vifo vya watoto njiti vinaweza kuepukika kwa silimia 75 iwapo jamii ikishirikiana na Serikali wataweka mkazo huduma za kinga, ugunduzi wa matatizo mapema na matibabu bora na kwa wakati stahili.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Ali Abdalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya mtoto Njiti yatakayofanyika tarehe 17 mwezi, mkutano huo ulifanyika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Daktari wa watoto Khamis Ali Abeid akitoa ufafanuzi wa masuala ya waandishi wa habari katika mkutano uliozungumzia maadhimisho ya mtoto njiti yatakayo fanyika tarehe 17 mwezi huu, mkutano huo ulifanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
Muuguzi Maryam Juma Bakari kutoka Hospitali Kuu ya Mnazimmoja akitoa shukrani kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
Waandishi wa habari Makame Mshenga wa Maelezo na Rahma Suleiman wa Gazeti la Nipashe wakifanya zoezi la njia muafaka ya kumpatia huduma ya kumbeba mtoto njiti ili apata joto la mzazi (kangaroo) katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Wizara ya Afya.Picha na Makame Mshenga.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017
yaani makala yote ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/zanzibar-kuadhimisha-siku-ya-mtoto.html
0 Response to "ZANZIBAR KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI NOVEMBA 17 /2017"
Post a Comment