title : RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO
kiungo : RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO
RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO
NA JOEL MADUKA, GEITA
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wakazi wa kijiji cha Kazibizyo na Bulama kutumia rasilimali walizonazo ili kuchochea maendeleo ya vijiji vyao.
Mhandisi Luhumbi aliyasema hayo katika uzinduzi wa ujenzi wa zahanati kwenye Kata ya Nga’nzo na Shule kwenye kijiji cha Bulama ili kuwaondolea wananchi tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo.Alisema matatizo mengi yanasababishwa na baadhi ya viongozi kutowajibika badala yake kuweka mbele maslahi binafsi.
“Shida kubwa wananchi tumefanya makosa mengi mno tumekuwa na viongozi bora viongozi sio viongozi bora viongozi ambao awawezi kuamasisha viongozi ambao kazi yao ni kula michango ya wananchi viongozi ambao fedha zikija wanaangalia kupiga kwanza hela ndio wanaleta yale makombo ambayo yanajenga vitu vibovu vibovu,Sasa viongozi wa namna hiyo hatuwezi kuwavumilia Geita,ni bora wafungashe virago watafute Mikoa mingine,kipindi hiki ni kipindi cha kazi kama unaona kazi ni ngumu achia bodi”Alisisitiza Luhumbi.
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kuchanganya mchanga kwenye shughuli ya ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kazibizyo wakati wa zoezi la uhamasishaji wananchi kujitolea katika uchangiaji wa maendeleo ya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na shule Wilayani Bukombe.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye yupo (Katikakati)Josephat Maganga akishirikiana na wananchi pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kufanya shughuli ya kuchanganya mchanga.
Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akishiriki kujenga msingi wa kujenga zahanati ya kijiji cha Kazibizyo Wilayani Bukombe pamoja na wananchi ambao wamejitokeza kuunga jitihada za serikali za kuleta maendeleo ya huduma za afya maeneo ambayo yanauwitaji .
Katibu tawala wa wilaya ya Bukombe akishiriki zoezi la ujenzi.
Hivyo makala RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO
yaani makala yote RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/rc-luhumbi-asisitiza-wananchi-kutumia.html
0 Response to "RC LUHUMBI ASISITIZA WANANCHI KUTUMIA RASILIMALI WALIZONAZO KUCHOCHEA MAENDELEO"
Post a Comment