title : TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI
kiungo : TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI
TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI
Na mwandishi wetu, Mwanza.
Wadau wa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (fish caging) mkoani Mwanza wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza tasnia iyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa samaki mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea kujionea maendeleo ya tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba mkoani Mwanza.
Bw. Mpanju alisema kuwa ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika tasnia hiyo mpya ya ufugaji wa samaki imekuwa inawapa changamoto katika uendelezaji wa tasnia hiyo yenye faida lukuki kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.
Bw. . Mpanju aliongeza kuwa ukosefu wa mikopo ya uhakika imekuwa inarudisha nyuma ukuaji wa tasnia hiyo mpya nchini kwa kuwa mahitaji mengi kwa ajili ya kuhudumia ufugaji wa samaki inapatikana nje ya nchi hivyo kuhitaji kiasi kikubwa cha mtaji.sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.
“Uduni na ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
Akijibu changamoto hizo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia) akiuelezea Ugeni kutoka TADB kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba.. wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati). Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Joseph Mutashubilwa (kushoto) na Bw. Dome Malosha (wapili kushoto).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akihoji masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba wakati alipouongoza ugeni kutoka TADB kutembelea Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza. Wanaomsikiliza ni Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Anuruphus Mpanju (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia).
Meneja Mradi wa Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju, Bw. Artem Ivanieiev (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kulia) kuhusu Shamba la Kutotoleshea vifaranga vya samaki vya Kampuni ya Mpanju.
Sehemu ya vizimba vya kukuzia samaki vinavyomilikiwa na Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI
yaani makala yote TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/tadb-yaombwa-kusapoti-wadau-wa-ufugaji.html
0 Response to "TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI"
Post a Comment