title : WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE
kiungo : WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE
WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.
Hayo amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.
“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka vituo vya Afya vya Serikali 524 viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya 265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya nyenzo za kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE
yaani makala yote WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/waziri-ummy-awataka-waganga-wakuu-wa_20.html
0 Response to "WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE"
Post a Comment