UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA
kiungo : UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

soma pia


UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

Benny Mwaipaja

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Benki ya Dunia.

Lengo la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.

Dkt. Mpango alisema kuwa Utafiti huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato, chakula na pengo baina ya matajiri  na maskini kuanzia kipindi cha mwaka 2013 hadi sasa.

“Takwimu zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka 2012” Alisema Dkt. Mpango.

Alisema pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi unavyokua hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.

“Nimefurahi kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460 kwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba kupitia zoezi hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana wapata 620 katika maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dkt. Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi 10,460.

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu namna utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kufunga mafunzo ya Wadadisi, na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, Mjini Dodoma.
 Wadadisi wa Takwimu za Utafiti  wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/2018, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), Mjini Dodoma.



Hivyo makala UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA

yaani makala yote UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/utafiti-mapato-na-matumizi-kaya-binafsi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UTAFITI MAPATO NA MATUMIZI KAYA BINAFSI WAANZA TANZANIA BARA"

Post a Comment