Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili

Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili
kiungo : Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili

soma pia


Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Hospitali ya BLK ya New Delhi, India imefanikiwa kufanya upasuaji wa kihistoria wa kupandikiza figo (Renal Transplant) ikiwa ni mara ya kwanza nchini.

Upandikizaji wa figo umefanywa na madaktari bingwa wa Mhimbili na Hospitali ya BLK Novemba 21, mwaka huu na taarifa za wataalamu hao zimeeleza upasuaji huo umekuwa wa mafanikio makubwa na kwamba utakuwa endelevu.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kufanyika kwa upasuaji huo ni moja ya mkakati wa Serikali wa kuendelea kuboresha na kuanzisha huduma bora za kibingwa nchini.

“Serikali inaendelea na juhudi za kuboresha huduma za afya nchini chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli zikiwamo za kibingwa nchini na kupunguza rufaa za wagonjwa wanaohitaji huduma hizo nje ya nchi,” amesema Ummy Mwalimu.

Amesema upasuaji figo katika Hospitali ya Muhimbili utasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo serikali imekuwa ikitumia kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji wa kihistoria wa kupandikiza figo ambao umefanyika Novemba 21, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni mara ya kwanza upasuaji huo kufanyika nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawrence Museru, Dkt. Rajesh Pande, Dkt Sunil na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya figo Muhimbili, Dkt. Jacqueline Shoo wakiwa kwenye mkutano huo leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Dkt. Rajesh Pande na Dkt Sunil wakifuatilia mkutano huo.

Wataalamu wa figo wa Muhimbili ambao wameshiriki katika upasuaji huo wa kihistoria wakiwa kwenye mkutano huo leo.



Hivyo makala Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili

yaani makala yote Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/upasuaji-wa-kihistoria-kupandikiza-figo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Upasuaji wa Kihistoria Kupandikiza Figo Wafanyika Muhimbili"

Post a Comment