title : Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha
kiungo : Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha
Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha
Na Karama Kenyunko.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasomea upya mashtaka, washtakiwa Harbinder Singh Sethi na James Burchard Rugema rila kwa kuwaongezea mashtaka na kufanya idadi yao kufikia 12.
Mapema mwezi uliopita, washtakiwa hao walipandishwa kizimbani hapo baada ya kusomewa mashtaka sita kabla ya leo kuwa 12.
Katika mashtaka hayo ambayo ni ya uhujumu uchumi yapo pia matano ya utakatishaji wa fedha na kuisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.
Mashtaka hayo ni, kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu , kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu kuisababishia Serikali Hasara na kutakatisha fedha.
Washtakiwa wamesomewa mshtaka yao mapya na wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Katika shtaka la kwanza inadaiwa, Rugemarila Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Imedaiwa kuwa, Oktoba 18,2011na Machi 19,2014 washtakiwa hao wakishirikiana na watumishi wa umma walitekeleza mtandao huo wa uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.
Aidha katika shtaka la tatu linalomkabili Sethi peke yake imedaiwa, Oktoba 10,2011 katika mtaa wa Ohio Ilala, akiwa na nia ya ulaghai alighushi fomu namba 14 a ya usajili wa makampuni na kuonyesha yeye ni mtanzania anayeishi Kitalu namba 887 Mtaa wa Mrikau Masaki wakati akijua ni uongo.
Seth pia anadaiwa kutoa nyaraka ya kughushi ambayo ni fomu namba 14a ya usajili wa kampuni kwa ofisa msajiri wa kampuni,Seka Kasera kwa njia ya kuonesha kwamba yeye ni mtanzania na Mkazi wa Mtaa wa Mrikau.
Mtuhumiwa James Burchard Rugemarila akirejeshwa rumande
Mtuhumiwa Harbinder Singh Sethi wakirejeshwa rumande.
Hivyo makala Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha
yaani makala yote Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/vigogo-iptl-rugemalira-na-habinder.html
0 Response to "Vigogo IPTL, Rugemalira na Habinder Sethi, waongezewa mashtaka, Sita ya utakatishaji wa fedha"
Post a Comment