TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa.

TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa.
kiungo : TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa.

soma pia


TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa.

Na.Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)mkoani Kilimanjaro,imemtia mbaroni Daktari wa Hospital ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi akituhumiwa kudai na kupokea rushwa ya shilingi 150,000.

Daktari huyo,Deogratias Godfrey Urio,alikamatwa jana katika mji mdogo wa Himo kwenye baa maarufu ya Mombasa High Way  baada ya kuwekewa mtego na makachero wa takukuru mkoani Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Kilimanjaro(RBC),Holle Makungu imesema kuwa kukamatwa kwa daktari huyo kunatokana na malalamiko ya ndugu wa mgonjwa aliyekuwa akipigwa dana dana kupatiwa huduma ya upasuaji katika hospital hiyo.

Makungu ameeleza katika taarifa yake kuwa,mgonjwa huyo alikuwa akihitaji kufanyiwa upasuaji wa uvimbe katika kizazi chake tangu oktoba mwaka huu baada ya kufanyiwa vipimo kwenye hospital hiyo na kubainika kuwepo kwa uvimbe.

Lakini licha ya kubainika kuwepo na uvimbe huo,mgonjwa huyo hakuweza kupata tiba haraka baada ya kuelezwa na daktari huyo kuwa hawezi kufanyiwa upasuaji huo hadi hapo atakapotoa fedha hizo.

Makungu ameeleza kuwa,baada ya taarifa hizo kuwafikia,mtego uliandaliwa na daktari huyo aliweza kutiwa mbaroni jana Novemba 15 akiwa kwenye baa hiyo ya Mombasa High Way.

“Tunaendelea na uchunguzi wa tuhuma hizo na atafikishwa mahakamani mara tu uchunguzi utakapokamilika,takukuru  inatoa rai kwa madaktari na wauguzi katika hospital ya Mawezi kuzingatia viapo vyao ili Mawenzi iwe hospital ya kuigwa kwa huduma bora”,amesema makungu.

Mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Kilimanjaro akahitimisha taarifa yake kwa kuonya kuwa kwa wale wachache watakaoendelea kutozingatia viapo vyao,watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na pia kuwataka waajiri wao wachukue hatua kali za kinidhamu dhidi ya watumishi hao .

Mwisho.



Hivyo makala TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa.

yaani makala yote TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/takukuru-kilimanjaro-yamshikilia_16.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAKUKURU Kilimanjaro Yamshikilia Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Kwa Tuhuma za Rushwa."

Post a Comment