title : SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA
kiungo : SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA
SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa wananchi wazalishe mazao ya Mihogo, Alizeti kutokana na kuwepo kwa masoko katika nchi ya China hali ambayo itafanya kufikia uchumi wa kati kwa kuingiza fedha za kigeni nyingi.
Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akizungumza katika kongamano la Kujadili fursa za Uwekezaji katika Ushirikiano kati ya Tanzania na China, zilizopo nchini lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mwijage amesema kutokana na kuwepo ushirikiano mzuri sana baina ya China na Tanzania Watanzania wanahitajika kuchangamka kwa kulima mazao ambayo yana soko katika nchi hiyo hivyo kufanya juhudi katika kilimo cha mazao ya Mihogo, Alizeti na Mafuta ya Pamba ni muhimu.
Amesema kuwa wanahitaji wawekezaji wa viwanda vya kuweza kuzalisha bidhaa za mazao ya kilimo na kuondoa uzafilishaji wa mazao ghafi ambapo inafanya kuona soko gumu.
Aidha amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na China ni wa siku nyingi hivyo lazima sasa tunyanyuke pamoja licha hatuwezi kuwafikia kama wao.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Watendaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na China ambalo limefanyika chuoni hapo leo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Isaria Kimambo akizungumza katika kongamano na Ushirikiano kati ya Tanzania na China katika kutumia fursa za uwekezaji ambao utaleta maendeleo nchini.
Sehemu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam.
Kwaya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ikiongoza uimbaji wa wimbo wa Taifa katika ufunguzi wa kongamano hilo.
Hivyo makala SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA
yaani makala yote SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/serikali-yahamasisha-kilimo-cha-mihogo.html
0 Response to "SERIKALI YAHAMASISHA KILIMO CHA MIHOGO ALIZETI KWANI KUNA SOKO LA UHAKIKA NCHINI CHINA"
Post a Comment