title : SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU
kiungo : SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU
SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU
Na Ismail Ngayonga- MAELEZO
SERIKALI ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la nchi hiyo (JICA) imesema itaendelea kuisadia miradi mikubwa ya maendeleo nchini ikiwemo barabara ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Hayo yamesemwa mwishoni wa wiki Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida wakati wa utoaji tuzo ya heshima ya Rais wa JICA kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale.
Balozi Yoshida alisema tangu mwaka 1980, JICA imekuwa mshirika wa karibu wa maendeleo na Serikali ya Tanzania ikiwemo kuunga mkono juhudi za kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi kupitia ufadhili wa miradi ya kipaumbele kwa ikiwemo barabara.
Aliongeza kuwa utoaji wa Tuzo ya Rais wa JICA kwa Mhandisi Mfugale imedhirisha imani ya Serikali ya Japan kwa Tanzania katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofadhiliwa JICA, na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.
“Misaada ya JICA nchini unajumuisha misaada bila masharti, misaada ya kiufundi, kufadhili miradi kwenye maeneo ya vipaumbele kwa serikali hususan katika sekta za kilimo, miundombinu ya barabara, maji, nishati, utawala na afya” alisema Balozi Yoshida.
Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa kupewa Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshinda (kushoto) akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patric Mfugale kwa mara baada ya kumkabidhi Tuzo ya Rais wa JICA mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo imetolewa kwa watu binafsi 23 dunia ikiwa ni kutambua michango yao katika kusimamia miradi ya JICA.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akionyesha Tuzo ya Rais wa JICA katika hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshinda, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Makamu wa Rais wa JICA Hiroshi Kato na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Toshio Nagase.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU
yaani makala yote SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/serikali-ya-japan-yaahidi-kuendelea.html
0 Response to "SERIKALI YA JAPAN YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU"
Post a Comment