title : NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU
kiungo : NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU
NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU
Waziri Mkuu. Kassim Majaliwa (mwenye Tai nyekundu) amefanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Dar es salaam leo November 29, 2017 na kubaini Kampuni ya NAS ikitaka kutoa Semi Trela 44 bila ya kufuata utaratibu.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro
kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya
Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya
semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu.
Pia
Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara
wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi
kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini.
“Mtu asije hapa aseme
amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia
Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata
taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe
hatua kwa mujibu wa sheria.”
Ametoa agizo hilo leo (Jumatano,
Novemba 29, 2017) alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata
taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka
kutoa magari hayo yaliyoingizwa nchini mwaka 2015 kutoka nchini
Uturuki.
Hatua hiyo imekuja baada ya Bw. Bahman wa kampuni ya
NAS kutaka kupata msamaha wa kodi kwa kuidanganya TPA kwa madai kwamba
wamewasiliana na Waziri Mkuu na wasipotekeleza jambo hilo watapata
matatizo.
Hivyo makala NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU
yaani makala yote NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/newz-alertwaziri-mkuu-abaini-semi-trela_29.html
0 Response to "NEWZ ALERT:.WAZIRI MKUU ABAINI SEMI TRELA 44 ZIKITAKA KUTOLEWA BANDARINI BILA YA KUFUATA UTARATIBU"
Post a Comment