title : MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI
kiungo : MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI
MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI
Serikali imesema imeweka mikakati endeleveu ya kupunguza vifo vya watoto njiti kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Neema Rusibamayila katika Siku ya Kimataifa ya Watoto Njiti ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 17.
“Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi mmoja hivyo kutokana na hali hii tunapaswa kudhibiti vifo kwa watoto wachanga,” alisema Dkt. Rusibamayila.
Alisema takwimu zinaonyesha asilimia 13 hadi 17 ya watoto wote wanaozaliwa Tanzania ni njiti na kwamba kutokana na hali hiyo Serikali kupitia Wizara ya Afya, imekuwa ikiratibu progamu mbalimbali za kupunguza vifo vya watoto wachanga na wa chini ya miaka mitano.
Mkurugenzi huyo alisema moja ya program hizo ni kumsaidia mtoto kupumua baada ya kuzaliwa, kupanua huduma za watoto wachanga kwa kujenga wodi za watoto wachanga katika hospitali za manispaa na wilaya pamoja na kutoa mafunzo kwa wa hudumu wa afya jinsi ya ya kuhudumia watoto wachanga.
Kaimu Mkuurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Janneth Mghamba akizungumza kwenye maadhimisho ya mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa Novemba 17 kila mwaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai.
Mkurugenzi wa Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akizungumza na kinamama pamoja na wataalamu wengine wa afya katika siku ya mtoto njiti duniani. Kulia ni Kaimu Mkuurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Janneth Mghamba, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Afya ya Uzazi na Mtoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Felix Bundara na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Watoto, Dkt. Merry Charles.
Baadhi ya kinamama wenye watoto njiti wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo Muhimbili.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI
yaani makala yote MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/muhimbili-yaadhimisha-siku-ya-mtoto.html
0 Response to "MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI DUNIANI"
Post a Comment