Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.

Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.
kiungo : Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.

soma pia


Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.

Na Estom Sanga – Iringa 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekani –USAID-bwana Andy Karas amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika kuwafikia wananchi wanaokabiliwa na umasikini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ambao umeanza kuonyesha mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali nchini, jambo linalovutia wadau wa maendeleo kuendelea kusaidia jitihada hizo. 

Bwana Karas ameyasema hayo alipokutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli katika halmashauri ya Wilaya ya Iringa ,mkoani Iringa ambako licha ya kuelezwa namna TASAF inavyoendelea kutekeleza Mpango huo, lakini pia alishuhudia namna walengwa wa mpango huo walivyoboresha maisha yao kwa kutumia fedha za ruzuku za mfuko huo. 

Amesema hamasa inayoonyeshwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kujiletea maendeleo kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwa kutumia fedha zinazotolewa na Serikali kupitia TASAF, imelivutia Shirika hilo na kuahidi kuwa litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha utaratibu wa kuwainua wananchi kiuchumi . 

Bwana Karas amesema utaratibu wa kuwafikia na kuwasaidia moja kwa moja wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ya kiuchumi umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani na umeonyesha mafanikio makubwa kwa kusisimua shughuli za kiuchumi na kijamii kwa kaya masikini . 

Aidha Mkurugenzi Mkazi huyo wa USAID amevutiwa na masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia TASAF hususani katika nyanja za elimu, afya, lishe na uwekezaji kwenye shughuli za kiuchumi kwa walengwa wa Mpango huo kuwa umeamusha ari ya kutokomeza umasikini miongoni mwao. 
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani USAID bwana Andy Karas akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini ambako akutana na walengwa wa Mpango huo kuona namna wanavyonufaika na Mpango huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID bwana Andy Karas akisoma taarifa kwenye mkutano wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini ambako alitembelea kuona namna walengwa wa Mpango huo wanavyonufaika na ruzuku inayotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi wilaya ya Iringa Vijijini wakiwaburudisha wageni kutoka Shirika la Misaada la Marekani –USAID waliotembelea kijiji hicho kuona shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF .
Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Misaada la Marekani Bwana Andy Karas akisalimiana na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Igingilanyi kata ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini wakati alipotembelea kijiji hicho.Katikati yao ni Mkurugenzi wa miradi wa TASAF bwana Amadeus Kamagenge.



Hivyo makala Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa.

yaani makala yote Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/mkurugenzi-mkazi-wa-usaid-bwana-andy.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mkurugenzi Mkazi wa USAID bwana Andy Karas atembelea walengwa wa TASAF mkoani Iringa."

Post a Comment