title : BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA
kiungo : BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA
BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA
Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetembelea mradi wa ufugaji wa vifaranga vya samaki unaotekelezwa na kikosi cha 822 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Rwamkoma wilaya ya Butiama kupitia Kiteule chake cha Bulamba, wilayani Bunda.
Akizungumza lengo la ziara hiyo, mkuu wa msafara huo ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila amesema lengo kubwa la kutembelea Mradi huo ni kujionea juhudi za serikali za kuchagiza mapinduzi ya kilimo hasa katika tasnia ya ufugaji na uvuvi wa samaki nchini.
Bibi Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini.
Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Kushoto ni Afisa Uvuvi wa wilaya ya Bunda, Bw. Steven Ochieng’.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Dome Malosha (kulia) akizungumza wakati walipotembelea Mradi wa Ufugaji wa Samaki kwa Vizimba Kiteule cha Bulamba uliopo wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Bw. Joseph Mutashubilwa (katikati).
Msimamizi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki wa JKT Kiteule cha Bulamba, Luteni Kelvin Gondo akitoa maelezo juu ya maendeleo ya ufugaji wa samaki katika hatua mbalimbali.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA
yaani makala yote BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/benki-ya-kilimo-yatembelea-miradi-ya.html
0 Response to "BENKI YA KILIMO YATEMBELEA MIRADI YA JKT KITEULE CHA BULAMBA, BUNDA"
Post a Comment