Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400
kiungo : Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

soma pia


Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

NAIBU Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewahamasisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini na kufanikisha kupata vifaa vya ujenzi wa mradi wa awamu ya kwanza wa nyumba za Polisi Mikoa ya Pemba, Zanzibar.

Mradi huo umeanza katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo nyumba kumi na mbili zinatarajiwa kujengwa ili kufanikisha askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi ndani ya mikoa hiyo waweze kuishi katika nyumba za jeshi pamoja na kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa nyumba za makazi ya polisi hao, pia mradi huo utajenga nyumba katika mikoa mipya nchini pamoja na makao ya nchi Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, katika Bandari ya Mkoani katika Mkoa wa Kusini Pemba, jana, Mhandisi Masauni alisema, ujenzi wa nyumba hizo utakua ni wa hatua ya awali, lakini mipango mbalimbali itaendelea kuwezesha nyumba nyingi zaidi kujengwa katika eneo hilo ili kuhakikisha baadhi ya askari wanaoishi nje ya kambi za polisi waweze kuishi kambini ili kuliwezesha Jeshi la Polisi kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa zaidi.

“Leo nimewakabidhi wakuu wa mikoa hawa vifaa vya ujenzi ambavyo ni mifuko ya saruji, nondo, ndoo za rangi na mabati ili waweze kusimamia zoezi hili la ujenzi wa nyumba za askari wetu kwa umakini mkubwa,” alisema Masauni na kuongeza;
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto) mabati yaliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya Meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, nondo zilizochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwajuma Majid Abdalla (kushoto), na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman, mifuko ya saruji iliyochangwa na wadau mbalimbali aliowatafuta Naibu Waziri huyo kwa lengo kuchangia ujenzi wa nyumba za makazi ya Polisi katika Mkoa wa Kusini Pemba na Kaskazini Pemba. Makabidhiano hayo ya mabati, mifuko ya saruji, ndoo za rangi pamoja na nondo yalifanyika ndani ya meli ya Azam Sealink katika Bandari ya Mkoani mara baada ya meli hiyo kuwasili na mizigo hiyo kutoka jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa Pemba pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada kukabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi wa nyumba za polisi katika Mikoa ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema wadau wamemchangia shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 12 za Jeshi la Polisi ili kukabiliana na ukosefu wa nyumba za polisi katika mikoa hiyo. Awamu ya ujenzi wa nyumba hizo ni ya kwanza, na awamu ya pili itakua mikoa ya mipya nchini ambayo ni Geita, Simiyu, Katavi na Songwe. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Mwajuma Majid Abdalla, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.



Hivyo makala Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400

yaani makala yote Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/masauni-ahamasisha-ujenzi-wa-nyumba-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba, wadau wajitokeza wamchangia milioni 400"

Post a Comment