title : KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY
kiungo : KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY
KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka Serikali ya Norway kwa Serikali ya Tanzania, Balozi Arild Oyen ambaye alifika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe maalum. Pamoja na mambo mengine walizungumzia namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Norway hususan katika sekta za Nishati, Elimu na Utamaduni. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 08 Novemba, 2017.
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Mkenda na Balozi Oyen (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni Bw. Jestas Nyamanga, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Bi. Ramla Hamis, Afisa Mambo ya Nje.
Mazungumzo yakiendelea. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanne Marie Kaarstad.
Prof. Mkenda na Balozi Oyen wakimsikiliza Balozi Kaarstad mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao
Prof. Mkenda akiagana na Balozi Oyen
Hivyo makala KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY
yaani makala yote KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/katibu-mkuu-wa-mambo-ya-nje-akutana-kwa.html
0 Response to "KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MJUMBE MAALUM KUTOKA NORWAY"
Post a Comment