title : DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA.
kiungo : DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA.
DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe amewapa siku 14 wataalamu wa ardhi wa Wilaya kuainisha mipaka baina ya Kata ya Misima iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Halmashauri ya Mji ili kuondoa mkanganyiko wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ameyazungumza hayo jana alipokuwa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Msomera Kata ya Misima baada ya uongozi wa Kijiji hicho kuomba msaada wa kusikilizwa ili kuainishiwa mipaka baina ya Kata na Vijiji ili kuondoa muingiliano.
Mh. Gondwe alisema kuwa wataalamuwa ardhi watapima na kuonesha mipaka baina ya Halmashauri ya Mji na Wilaya ili wafahamu mipaka yao na kutambua wanapaswa kuitika wapi na kuondoa migongano inayokwamisha wananchi kushiriki katika maendeleo.
Alisema kuwa Msomera ni Kijiji kilichoanzishwa kisheria na kipo kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi hivyo wananchi wote wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kuwataka wananchi wote wanaokuja kwenye Kijiji hicho na maeneo mengine kufuata masharti ya maeneo husika kwani Tanazania ni huru kuishi kwa kila mwananchi isipokuwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akizungumza na wafugaji wa Kijiji cha Msomera na akiwasisitiza kuwa Kuwa Kijiji hicho ni cha wafugaji wote bila kujali kabila.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe akiwaeleza wafugaji wa Kijiji cha Msomera kuwa wakulima kuingia kwenye eneo la kufugia mifugo kunatokana na baadhi ya viongozi kutokuwa waadilifu kwa kuuza maeneo bila kufuata taratibu na kuwataka kushirikisha wananchi kwa kila jambo kwani viongozi sio watu wenye maamuzi ya mwisho.
Baadhi ya wafugaji na wakulima walioshiriki mkutano wa hadhara.
mmoja wa wafugaji akitoa malalamiko yake kuhusu wakulima kuvamia eneo la mifugo na kuanza kulima kinyume na taratibu na kuomba kuanishiwa mipaka kuepuka muingiliano.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Hivyo makala DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA.
yaani makala yote DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/dc-handeni-atoa-siku-14-wataalamu-wa.html
0 Response to "DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA."
Post a Comment