CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI

CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI
kiungo : CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI

soma pia


CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI

Na Pamela Mollel,Monduli

Katibu Mkuu wa wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt Florens Turuka amesema kuwa jeshi hilo hivi sasa limejipanga katika kukabiliana na changamoto za ulinzi na usalama kwa kuwapatia askari wake mafunzo maalumu ya sayansi ya kijeshi. 

Aliyasema hayo Jana wakati akizungumza katika uzinduzi wa shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi inayotekelezwa na chuo cha uhasibu Arusha kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA). 

Alisema kuwa, kumekuwepo na matishio mengi ambayo yamekuwa yakijitokeza Kwa namna tofauti ambapo hivi sasa matishio hayo yamegeuka na kuhamia kwenye mitandao, hivyo kama jeshi wana wajibu wa kujipanga zaidi kwa kuwaandaa maaskari ili waweze kukabiliana na hali hiyo mahali popote. 

Dkt Turuka alisema kuwa, wao Kama jeshi ni wajibu wao kujipanga mapema kwa kuangalia namna ya kuwajengea uwezo hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia ili kuboresha ulinzi na usalama hapa nchini. 

Kwa upande wa Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo alisema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa maaskari wake kulingana na mabadiliko ya kidunia hasa katika maswala ya sayansi na teknolojia kwani ni eneo ambalo linahitaji elimu kubwa zaidi.  Alisema kuwa, ni lazima wasonge mbele na kwenda na wakati kwani wasipofanya hivyo watabaki nyuma na kamwe hawataweza kukabiliana na vitisho vilivyopo hivi sasa. 

Naye Mkuu wa chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli (TMA), Dokta Paul Massao alisema kuwa, wamekuwa wakitoa masomo ya kijeshi na kiraia ili kuwaandaa vijana katika hatua ya ngazi za juu zaidi kielimu ambapo kwa kuanzia kozi hiyo watahiniwa 158 wataanza kozi hiyo mapema. 

Kwa upande wa Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi alisema kuwa, mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia ambayo yamekuwa yakileta manufaa makubwa Sana. 
Mkuu wa majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akitoa hotuba fupi katika hafla fupi ya uzinduzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo mapema jana.
Meja jenerali Paul Peter Masao ambaye ni mkuu wa chuo cha mafunzo ya maafisa wanafunzi jeshi la ulinzi la Tanzania(TMA) akizungumza kwenye hafla hiyo jana.
Katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa Florens Turuka akizungumza katika uzinduzi wa uzinduzi wa shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo
Kaimu mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha, Dokta Faraji Kasidi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema mahusiano kati yao na chuo hicho cha kijeshi yameanza muda mrefu ambapo wao wamekuwa wakifundisha askari hao mafunzo ya kiraia.
kushoto aliyevalia suti ni Profesa Johannes Monyoambaye aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA)
Wanafunzi wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi iliyofanyika chuoni hapo mapema jana.
Picha ya pamoja.




Hivyo makala CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI

yaani makala yote CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/chuo-cha-mafunzo-ya-kijeshi-monduli.html

Subscribe to receive free email updates:

1 Response to "CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI CHAZINDUA KOZI MPYA YA SAYANSI YA KIJESHI"

  1. Dating for everyone is here: ❤❤❤ Link 1 ❤❤❤


    Direct sexchat: ❤❤❤ Link 2 ❤❤❤

    lR..

    ReplyDelete