AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA

AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA
kiungo : AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA

soma pia


AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA

Imeandikwa na Rais wa Taifa la Palestina, Mheshimiwa Mahmuud Abbas
Waingereza wengi hawamjui “Sir.Arthur James Balfour”ambae aliwahi kuwa Waziri Mkuu mwanzoni mwa karne ya ishirini, lakini jina lake ni maarufu sana kwa Wapalestina wapatao milioni kumi na mbili. Katika kumbukumbu ya azimio la Balfour,serikali ya Uingereza inalazimika kutumia fursa hiyo ili kurekebisha makosa ya kihistoria iliyoyafanya dhidi ya wananchi wetu wa Palestina.

Mnamo Novemba 2,1917 akiwa ofisini kwake mjini London,“Sir.Arthur James Balfour”alisaini barua akiliahidi shirika la kizayuni, kuanzisha taifa lao ndani ya ardhi ya Palestina. Ameahidi kutoa ardhi hiyo wakati sio yake, huku akifumbia macho haki za kisiasa za Wapalestina walioishi katika ardhi hiyo kwa miaka mingi. Kwa Wapalestina ambao ni raia wangu, matukio yaliyosababishwa na barua hii yamekuwa na uharibifu mkubwa, huku pia yakiacha madhara ya muda mrefu kwa wananchi wetu.

Sera ya Uingereza iliyounga mkono uhamaji wa Wayahudi kwenda Palestina, ikiwa ni mbadala wa kukataa kwao haki ya Kiarabu ya Palestina ya kujipangia mustakabali wao, sera hiyo imeleta mvutano mkali kati ya wahamiaji wa Kiyahudi wa Ulaya na wakazi wa asili wa Kipalestina. Palestina iliyokuwa ajenda ya mwisho ya kumaliza ukoloni, inasumbuka kama tunavyosumbuka wananchi wake kutafuta haki yetu isiyo badilika katika kujipangia mustakabali, jambo ambalo ni janga kubwa mno kushuhudiwa na historia ya sasa.

Mnamo mwaka 1948, wanajeshi wa kizayuni waliwafukuza kwa mabavu kutoka katika miji yao, watu wanaofikia milioni moja wakiwemo wanawake na watoto, huku wakifanya mauaji ya kutisha na kubomoa kabisa vijiji kadhaa. Wakati tulipofukuzwa kwa mabavu kutoka mji wa Safad, umri wangu ulikuwa miaka kumi na tatu, wakati Israel ikisherehekea kuasisi taifa lake, sisi Wapalestina tunakumbuka siku ya giza zaidi katika historia yetu. 

Azimio la “Balfour” kwa hakika sio tukio la kusahaulika, kwani wananchi wangu leo wanaofikia zaidi ya milioni kumi na mbili wamesambaa duniani kote, baadhi yao wakilazimishwa kwa nguvu kuacha miji yao mnamo mwaka 1948, huku zaidi ya Wapalestina milioni sita bado wanaishi uhamishoni hadi leo hii, waliosalia katika miji yao ni milioni (1.75) ila wao wanaishi chini ya mfumo wa kibaguzi uliopangika nchini Israel.

Aidha, Wapalestina zaidi ya milioni (2.9) wanaishi Ukingo wa Magharibi wakiwa chini ya uvamizi wa kijeshi na wa kinyama uliogeuka kuwa ni ukoloni. Miongoni mwao wapo wakazi wa Jerusalem ambao ni wa asili kabisa wapatao laki tatu (300,000), bado wanapambana na sera za kivamizi za Israel zinazowahamisha kwa nguvu kutoka katika mji wao. Huku wapalestina wengine wapatao milioni mbili wapo katika Ukanda wa Gaza, ambayo ni gereza la wazi linaloharibiwa mara kwa mara na vifaa vya jeshi la Israel.


Hivyo makala AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA

yaani makala yote AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/azimio-la-balfour-sio-mnasaba-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AZIMIO LA “BALFOUR” SIO MNASABA WA KUSHEREHEKEA"

Post a Comment