Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa

Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa
kiungo : Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa

soma pia


Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa




Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka wananchi kuzingatia Sheria wakati wa ujenzi wa makazi yao ili kuepuka kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa jambo linalosababisha bomoa bomoa isiyo ya lazima.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Angelina Mabula aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi duniani ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Karimjee.

Mhe.Mabula alisema kuwa ni vyema wananchi wazingatie sheria kabla hawajaanza kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi husika ili kuepuka ukiukwaji wa Sheria za nchi katika ujenzi wa makazi.
“Watanzania tunakumbushwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi kwa sababu ubomoaji unaofanyika siyo kwa makusudi bali ni kwasababu tu watu wamekiuka Sheria zilizopo na pengine watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali ambao wanawapa watu maeneo pasiporuhusiwa”, alisisitiza Mhe. Mabula

Akizungumuzia mpango mkakati wa Wizara hiyo Mhe. Mabula alisema kuwa zaidi ya Miji 26 nchini ikiwemo Mtwara, Singida Mwanza na Dar es Salaam iko kwenye mchakato wa kupangilia makazi yake na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya msongamano wa makazi.
 
Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula akihutubia katika hafla ya maadhimisho ya 32 ya makazi duniani kutoka kulia ni mkurugenzi wa nyumba Bw.Pius Tesha na wa pili kulia ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala maadhimisho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
PICHA 1
Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba kulia akitoa salam kwa Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula wa kushoto  katika maadhimisho ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.
PICHA 2
mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala kushoto akitoa maelezo kwa wadau wa nyumba na makazi katika maadhimisho ya 32 ya makazi duniania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo ya makazi Mhe. Angelina Mabula na wa pili kushoto ni Mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo cha ushirika moshi Dkt.Lucas Mataba.



Hivyo makala Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa

yaani makala yote Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/watanzania-watakiwa-kufuata-sheria-na_2.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Watanzania Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu Za Ujenzi kuepuka Bomoabomoa"

Post a Comment