title : WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA
kiungo : WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA
WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda , akizungumza na baadhi ya waumini baada ya kumaliza uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge.
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda, akizungumzia umhimu wa kutumia NHIF wakati wa uzinduzi wa huduma ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge.
Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki akiendelea kutoa maelezo ya umhimu ya mfuko huo kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge.
Bbaadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge.
SPIKA Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko ya Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda azindua huduma ya “TOTO AFYA KADI” kwenye nyumba za ibada.
Akizungumza na waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge amesema huduma hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 kwa Sh. 50,400 kwa mtoto mmoja kwa mwaka.
Makinda amesema kampeni hizo ambazo zitaendelea kwenye Madhehebu ya Dini lengo ni kuwa rafiki na huduma hiyo ili kufikia mwaka kesho watanzania asilimia zaidi ya 80 wawe wamejiunga na huduma hiyo.
Makinda amesema kiasi hicho cha Sh. 50,400 kitakachochangiwa kwa mwaka kitamuwezesha mwanachama huyo kupata matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.
Naye Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki amesema fao hilo pia hutolewa kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu kwa Sh. 50,400.
Pia amesema NHIF hutoa huduma kwa vikundi vya wajasiriamali walio kwenye vikundi vya watu kuanzia 10 kwa Sh. 76,800 kwa kila mwanachama mmoja ambaye atachangia fedha hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hivyo makala WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA
yaani makala yote WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wapeni-watoto-furaha-ya-maisha-kwa-kadi.html
0 Response to "WAPENI WATOTO FURAHA YA MAISHA KWA KADI ZA NHIF:MAKINDA"
Post a Comment