WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.

WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.
kiungo : WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.

soma pia


WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.

Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

WALENGWA wa Mpango wa kunusuru kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) wametakiwa kuanzisha vikundi vya ufugaji kuku ili waweze kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya kutafuta dawa za chanjo zitakazowasaidia kukabiliana na ugonjwa wa mdodo na kideri(Newcastle diasese) ambao umekuwa ukiwasababishia hasara.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Richius Bilakwata kwenye mikutano na walengwa wa vijiji vya Itebulanda na Nsenda wilayani Urambo.

Alisema kuwa ili waweze kuepuka kupata hasara kutokana na kuku zao kushambuliwa na ugonjwa huo ni vema wakawa wananunua chanjo na kuwachanja.“Moja ya chanjo inaweza kuchanja kuku wengi kwa pamoja ni vema mkajiunga pamoja ili muweze kuchangia katika ununuzi wa dawa hiyo kwa urahisi” alisema Bilakwata.

Aliwashauri walengwa kuwa wakati mpango huu wa kunusuru kaya ukielekea mwishoni ni vema wakajitihidi kutumia kipato kidogo wanachokipata kuwekeza katika miradi midogo kama vile ufugaji wa bata, kuku, mbuzi na mifugo mingine.

Bilakwata alisema kuwa miradi hiyo itawasaidia wakati mpango huo utakapokuwa umekoma.Nao walengwa wengi walisema kuwa wamekata tama kuendelea na ufugaji wa kuku kwa sababu ya kushambuliwa na magonjwa kama vile mdodo na kideri.

Hivi sasa kuku moja katika maeneo ya Urambo mjini anauzwa kwa wastani wa shilingi elfu 8 hadi elfu 12.


Hivyo makala WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU.

yaani makala yote WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/walengwa-wa-tasaf-watakiwa-kujiunga.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WALENGWA WA TASAF WATAKIWA KUJIUNGA PAMOJA KUKABILIANA MAGONJWA YA KUKU."

Post a Comment