Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti

Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti
kiungo : Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti

soma pia


Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti

Na Greyson Mwase, Simiyu

Wachimbaji wa madini ya dhahabu katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kufanya utafiti wa madini katika maeneo yao ili waweze kuwa na uhakika wa uchimbaji wa madini na uzalishaji wao kuwa na tija.

Wameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba, 2017 katika ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu yenye lengo la kukusanya kero za wananchi mbalimbali hususan katika shughuli za uchimbaji madini.

Akizungumza kwa niaba yao, Sylivester Fundikira alisema kuwa wameunda jumla ya vikundi 30 ambapo kila kikundi kina mashimo yake na kueleza kuwa wamekuwa wakipata changamoto ya upatikanaji wa madini ya uhakika kutokana na maeneo yao kutofanyiwa utafiti kwa muda mrefu.

Akijibu kero hiyo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisema kuwa Wizara ya Madini kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) imekuwa ikifanya tafiti sehemu mbalimbali nchini na kusisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo tayari kuwasaidia.

Alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini na kuongeza kuwa imeweka mikakati ya kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia vifaa kupitia ruzuku ili uchimbaji wao uwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

“ Tuna mpango wa kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinakuwa na mchango mkubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo tutahakikisha tunasimamia ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa mazingira ya uchimbaji madini yanakuwa rafiki,” alieleza Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo alisema kuwa kazi yake pamoja na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakua kwa kasi na kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Alisema kuwa sekta ya madini imekuwa na changamoto kubwa hususan katika upotevu wa mapato kutokana na wawekezaji wasio waaminifu na kukwamisha juhudi za serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Aliendelea kusema kuwa tangu Rais John Magufuli ameanza kupambana na wezi wa rasilimali za madini kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwa uzalishaji na mapato umebadilika kutokana na Serikali kuhakikisha kiwango sahihi kinapatikana na kulipiwa kodi serikalini.

Alisema Serikali imeweka Sheria Mpya ya Madini ya mwaka 2017 na kuwataka wachimbaji madini nchini kufuata sheria hiyo pamoja na kanuni zake.
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akijibu kero mbalimbali za wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Seif Shekalaghe akifafanua jambo mbele ya wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara.
Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini, Sylivester Fundikira akiwasilisha kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani).
Sehemu ya wakazi wa kitongoji cha Mwanguhi kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara.


Hivyo makala Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti

yaani makala yote Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wachimbaji-madini-maswa-waomba-maeneo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wachimbaji madini Maswa, waomba maeneo yao kufanyiwa utafiti"

Post a Comment