Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo

Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo
kiungo : Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo

soma pia


Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo

Vijana nchini wametakiwa kujiajiri kupitia kilimo badala ya kukimbilia nchi za nje kama njia ya mkato ya kutafuta maisha. Wito huo umetolewa na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakati akiyafunga rasmi maonesho ya siku ya chakula duniani yaliyofanyika kitaifa huko Kizimbani, Wilaya ya Magharibi A.

Amesema ni aibu kuona vijana wengi wa Kiafrika wanapoteza maisha baharini Mediterrania kwa safari za kwenda ulaya kutafuta maisha wakati Bara la Afrika lina fulsa nyingi za ajiri kupitia sekta ya kilimo. Akizunzungumzia kuhusu mikopo kwa wakulima wadogo wadogo Balozi Seif amezitaka taasisi za fedha nchini kutoa mikopo nafuu kwa wakulima hao kama hatua ya kuiunga mkono serikali ya kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini.

Amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuazisha viwanda vidogo vidogo vinavyotumia mali ghafi ya kilimo kutoka hapa nchini jambo ambalo litawasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa wingi na kujiongezea kipato chao.

Kuhusu maonesho Makamo wa Pili wa Rais ameipongeza Wizara ya Kilimo kwa maandalizi mazuri yaliyopelekea wananchi wengi wa Zanzibar kuhudhuria maonesho hayo. Amesema Serikali imejipanga kuyafanya maonesho ya kilimo hapa nchini kuwa endelevu na kuzitaka taasisi zinazohusika ikiwemo wizara ya Kilimo kuliendeleza eneo hilo la Kizimbani kwa kuweka miundo mbinu ya kudumu. 

Wakati huo huo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametowa zawadi ya kikombe kwa Jeshi la Kujenga Uchumi kwa kuwa mshindi wa Kwanza wa maonesho ya siku ya chakula duniani mwaka huu hapa Zanzibar.

Kutokana na ombi la wananchi wengi maonesho hayo ya kilimo yataendelea kwa siku moja zaidi ili kutoa nafasi kwa wananchi kufaidika na taaluma ya kilimo inayotolewa pamoja na kununua bidhaa mbali mbali za kilimo.

Aidha Serikali imekusudia kutoa fursa kwa wakulima kuuza bidhaa zao kila wiki katika eneo hilo la maonesho ili kutoa fursa kwa wakulima kuwapatia soko la uhakika.
Balozi Seif akiangalia zana za kilimo. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeongeza ununuaji wa zana za kisasa za kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Balozi Seif akipata maelezo kuhusu ufugaji wa mbuzi wa kisasa.


Hivyo makala Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo

yaani makala yote Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/vijana-nchini-watakiwa-kujiajiri.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Vijana nchini watakiwa kujiajiri kupitia kilimo"

Post a Comment