title : USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE
kiungo : USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE
USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE
Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu limeendelea leo mkoani Songwe, ambapo zaidi ya Kata 5 tayari zimekamilisha Usajili huo uliolenga kukusanya taarifa sahihi za watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakiwemo wageni wanaoishi kihalali mkoani humo.
Wakazi wa Songwe na Mbozi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kunufaika na manufaa mapana ya Kitambulisho hicho na pia kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora zaidi.
Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Ndugu Eckson Mwakyembe akiwa na Mtendaji wa Kijiji cha Mlowo Bi. Judith Mtega wakikamilisha fomu za maombi ya Usajili za wananchi wa vijiji vya Shuleni, Mtakuja, Mlowo na Kiwandani kata ya Mlowo wakati zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa likiendelea wilayani humo.
Meneja Mifumo ya Komputa wa ndugu Francis Saliboko akifanyia matengenezo ya kiufundi moja ya kifaa kinachotumika wakati wa usajili katika zoezi linaloendelea Kata ya Mlowo – Mbozi mkoani Songwe.
Maafisa Usajili wa NIDA wakifanya kazi ya kupiga picha na kuchukua alama za kibaiolojia katika zoezi linaloendelea kata ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Afisa Usajili Bi. Coletha Peter na Bi. Magreth Moshi wakisaidia taratibu za kuchambua na kuhakiki fomu za maombi ya Vitambulisho za wananchi wa kata ya Mlowo kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kupiga picha, kuchuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.
Mwananchi wa kata ya Mlowo akichukuliwa alama za vidole, picha na kuweka saini ya kielektroniki wakati wa Usajili Vitambulisho vya Taifa. kushoto ni Afisa Usajili Ndugu Baraka Haonga.
Hivyo makala USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE
yaani makala yote USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/usajili-vitambulisho-vya-taifa-mkoa-wa.html
0 Response to "USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA SONGWE"
Post a Comment