TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA

TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA
kiungo : TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA

soma pia


TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA

Mmoja wa viongozi wa Chama cha watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania(TAS) Rehema Athuman ( kulia) akimjulia hali Mzee Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga, Kata ya Kisaki, wilaya ya Morogoro ambaye alikatwa sehemu ya mkono wake wa kushoto ambaye juzi aliletwa kutoka kituo cha Afya Duthumi na kulazwa hosipitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kuendelea na matibabu zaidi. ( Picha na John Nditi).

Na John Nditi, Morogoro

CHAMA cha watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania(TAS) kimewaomba  viongozi wa dini, siasa na wadau mbalimbali kujikita kutoa elimu kwa wananchi  ili waweze kubadili mitazamo na kuacha kuwadhuru  wenye ualbino  kutokana na imani za kishirikina  na wambue  nao ni binadamu sawa na  walivyo wengine.

Mwenyekiti wa TAS Taifa, Nemes Temba  alisema hayo hivi karibuni ( Okt 5)  mjini hapa baada ya kumjulia hali mwenzao Nassoro Msingili (75) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyarutanga,  Kata ya Kisaki , wilayani Morogoro  mwaka huu baada ya kufanyiwa ukatili  Oktoba 3, mwaka huu na baadhi ya  watu kumkata mkono  wa kushoto na kutokomea nao.

Temba alisema,   kitendo cha Mzee Msingili kukatwa mkono kimewaumiza  wao kama  watu wenye ualbino na taifa kwa ujumla na kukemea  vikali  kitendo hicho kwa kuwa kufuatia tayari ameongezewa  ulemavu mwingine zaidi ya ualbino aliokuwa nao.

Alisema kuwa  kwa wastani asilimia kubwa  ya  suala la mauaji, kukatwa viungo na kunyanyaswa kwa watu wenye ualbino ni ya kishirikina   ambao unapaswa kukemewa na kupingwa vita na kila Mtanzania.

Hivyo alimwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk  John  Pombe Magufuli  kulitolea tamko la kukemea vikali vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino nchini ili waweze kuishi kwa  amani sawa na watanzania wengine.

waandishi wa Habari mjini Morogoro  juu ya wao kukemea vikali kitendo cha ukatili alichofanyiwa albino mwenzao Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga Kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro vijijini Oktoba 3 mwaka huu.

“ Natoa  wito kwa viongozi wa dini, siasa na wadau mbalimbali  washiriki kutoa elimu kwa wananchi  ili wabadili  mitazamo na kuacha kuwadhuru albino kwa imani za kishirikina  na badala yake atambue  kuwa  albino nao ni binadamu kama walivyo watu wengine” alisema Temba.

Hata hivyo aliiomba Serikali kufanya jitihada kwa kushirikiana na wadau wengine kuweza kupata takwimu sahihi za ualbino ili kuweza  kuwalinda  na kupatia huduma muhimu .

Msingili (75) alikatwa mkono wa kushoto mnamo Oktoba 3 ,mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika kijiji cha Nyarutanga , kata ya Kisaki,  wilayani Morogoro baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana  wakati akiwa amelala nyumbani ,na kulazwa  katika Kituo cha afya Duthumi  ambapo juzi alihamishiwa  Hospitali ya Rufaa  ya mkoa wa Morogoro  kwa  ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Akizungumza na gazeti hili juzi , akiwa wodi ya majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Msingili alisema kuwa wakati akivamiwa usiku alikuwa peke yake kwa kuwa ndugu zake walikuwa wamehamishia makazi ya muda shambani  kuvuna nafaka.

Alisema kuwa akiwa amelala usiku watu wasiofahamika walimvamia nyumbani kwake na walimpiga na kitu butu kama rungu kichawani na alipojihami kwa kuinua mgomo wake wa kushoto juu ghafla akikatwa na panga na  watu hao kutokomea na sehemu ya mkono wake wa kushoto.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonce Rwengasira,alisema kufuatia tukio hilo Polisi inawashirikia watu wawili kwa tuhuma hizo ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili upelelezi bado unendelea kufanyika na watafikishwa mahakamani wakati wowote ule.


Hivyo makala TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA

yaani makala yote TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/tas-taifa-waomba-elimu-itolewe-kulinda.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA"

Post a Comment