title :
kiungo :
Na Mathias canal, Singida
Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.
Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.
Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.
Akizungumza na Mtandao wa http://ift.tt/2qZnn1l Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.
Alisema kuwa pamoja na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa CCM Wilaya lakini pia nafasi zingine zilizowaniwa ilikuwa ni pamoja na Nafasi Ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ambapo Richard ni Ntandu aliibuka mshindi kwa kupata kura 61, nafasi ya pili ni Khamisi Swalehe Kimu kura 35, Iddi Athumani Monko kura 8 na Swalehe Munkumbu Sungi aliyepata kura 3.
Nafasi ya Halmashauri Kuu ya Wilaya waliogombea ni 27 ambapo kati yao walioshinda ni Sabasaba Manase, Edward Jared Ihondo, Japhet Ntandu Gham, Justin Joseph Monko, Mohamed Abdallah Ghamayu, Nkumbi Mohamed Kemi, Zuena Dunya, Simon Mumbai, Shabani Ally Mang'ola, na Wiliamu Mwang'imba Nyaland.
Nafasi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa waliomba walikuwa watano lakini washindi kati yao ni Mchungaji Wilson Mtatuu Ihucha, na Sada Njiku. Wajumbe wa Kamati ya siasa Wilaya ni Sabasaba Manase, Shaban Mang'old na Edward Jared Ihonde.
Katibu huyo wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa huu ni wakati wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchama na viongozi wote waliochaguliwa ili kuongeza ufanisi na nguvu ya chama katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Jumla ya wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo ni 788 kati ya wajumbe 845 wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini
MWISHO
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/katibu-wa-chama-cha-mapinduzi-ccm.html
0 Response to " "
Post a Comment