title : RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE.
kiungo : RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE.
RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE.
Mwambawahabari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amekagua ujenzi wa Jengo la Huduma Dharura ya kwenye Hospital ya Rufaa Temeke ambayo Ujenzi wake unafadhiliwa na Ubalozi wa Japan Nchini Tanzania
Ujenzi wa Jengo hilo unagharimu kiasi cha Shillingi Million 800 ambazo ni matunda ya jitiada binafsi za RC Makonda baada ya kumtafuta Balozi wa Japan Nchini Tanzania na kumueleza changamoto ya ukosefu wa kitengo cha Huduma za haraka kwenye Hospital za Mkoa ambapo baada ya mazungumzo Balozi alipokea kwa mikono miwili ombi la RC Makonda.
RC Makonda, amesema kukamilika kwa jengo hilo itasaidia kupunguza Vifo vitokanavyo na Wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka kuikosa huduma hiyo kwa uharaka.
Amesema jengo hilo ni mahususi kwajili ya wagonjwa wote wanaohitaji huduma ya haraka hususani Majeruhi wa Ajali, Wanaougua Malaria kali ya gafla, Maumivu ya Tumbo, wanaobanwa na Kifu, Wajawazito, Homa kali, ajali ya Moto na Magonjwa yote yanayohitaji huduma ya haraka.
Amebainisha kuwa wagonjwa wanaohitaji huduma ya haraka wanaofikishwa Hospitalini hapo wamekuwa wakipelekwa Hospital ya Muhimbili ambako ni mbali kutoka Temeke hivyo kusababisha wengi wao kupoteza maisha Barabarani.
Aidha Makonda, amesema baada ya kumalizika kwa jengo hilo ujenzi wa majengo ya huduma ya haraka utahamia kwenye Hospital ya Amana na Mwananyamala ilikuipungizia mzigo Muhimbili
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Temeke Dr. Aman Malima amesema kwa siku wanapokea wagonjwa kati ya 1,800 -2,000 ambapo kati ya hao 200 ni wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura hivyo amesema uwepo wa huduma hiyo itasaidia kuokoa maisha.
Amempongeza RC Makonda kwa juhudi zake binafsi za kutafuta wadau waliofanikisha ujenzi wa Jengo hilo.
Nae Mkandarasi wa ujenzi huo Bwana Abdulkadir Msangi amesema ujenzi umefikia 85% ambapo hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi November ujenzi utakuwa umekamilika na jengo kukabidhiwa.
Hivyo makala RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE.
yaani makala yote RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/rc-makonda-akagua-ujenzi-wa-jengo-la.html
0 Response to "RC MAKONDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA HUDUMA ZA DHARULA HOSPITAL YA TEMEKE."
Post a Comment