Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi

Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi
kiungo : Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi

soma pia


Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi




Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, Oktoba 14, 2017

Wahandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), akifanyia matengenezo moja ya mashine za kufua umeme kwenye kituo cha kufua umeme Mtwara, leo Oktoba 14, 2017


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, Mtwara
WAHANDISI na mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wanapambana usiku na mchana kuzifanyia matengenezo mashine za kufua umeme, ili kuondoa tatizo la kukosekana kwa umeme kwa vipindi virefu kila siku kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.


Akizungumza mjini hapa leo Oktoba 14, 2017, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia Uzalishaji, Mhandisi Kaitwa Bashaija, (pichani juu), amesema kwa sasa Wahandisi na mafundi wa shirika hilo wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana ili kutengeneza mitambo hiyo na hivyo kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.


K-VIS BLOG ilishuhudia mafundi hao wakifanyakazi ya kurekebisha mitambo hiyo katika kituo cha kuzalisha umeme wa kutumia gesi asilia mkoani Mtwara leo Oktoba 14, 2017.


“Mitambo hii ina kiasi cha mika 10 tangu ifungwe, na kadiri miaka inavyokweda ndivyo ongezeko la uhitaji wa umeme hususan mkoani Mtwara linazidi kuongezeka kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi,” Alisema Mhandisi Bashaija.


Alisema, miaka michache iliyopita baadhi ya mitambo iliweza kuzimwa na bado hali ya umeme ilikuwa imara.Wiki iliyopita Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani aliagiza TANESCO kufanya juhudi za ziada kuhakikisha tatizo la umeme mkoani Mtwara na Lindi linapatiwa ufumbuzi wa haraka.


Kutokana na hali hiyo Naibu Mkurugenzi huyo wa TANESCO, alisema kuwa kwa sasa wana mipango ya muda mfupi na mrefu katika kuhakikisha wanaimarisha miundombinu ya umeme katika mikoa ya kusini.


Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, alisema kuwa licha ya changamoto hiyo kwa sasa bado mitambo iliyopo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme katika mikoa hiyo.


“Pamoja na hali hii lakini kwa sasa tunakwenda vizuri kiasi ila si sana maana umeme kuna wakati unarudi na kukatika. Na tunaamini tutafanikiwa kurudi katika hali ya kawaida na kikubwa tunawaomba wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kutuvumilia kwani nasi tunajua umuhimu wa umeme katika shughuli za uzalishaji.” Alitoa rai Mhandisi Chinumba.





Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, akizungumzia hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka.







Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia mkoani Mtwara Oktoba 14, 2017.









Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia zualishaji umeme, Mhandisi Costa


Msanifu gazeti wa gazeti la Mwananchi, Bi. Lilian Timbuka akiuliza swali.

Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa kutumia gesi asilia cha Mtwara, Mhandisi Mkulungwa Chinumba, akizungumzia hatua zinazoendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi wa haraka. Kulia ni Mhandisi Bashaija.


Hivyo makala Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi

yaani makala yote Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/nishati-wahandisi-wa-tanesco-wapambana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Nishati : Wahandisi wa TANESCO Wapambana kurejesha Umeme mikoa ya Mtwara na Lindi"

Post a Comment