title : Ni Wakenya Rock City Marathon 2017
kiungo : Ni Wakenya Rock City Marathon 2017
Ni Wakenya Rock City Marathon 2017
Abrahamu Too kutoka Kenya ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19
Kivutio katika mbio hizo ilikuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ambae mbali na kuzindua mbio hizo pia alishiriki katika mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.
Nafasi ya tatu katika mbio hizo pia ilichukuliwa Mkenya George Onyacha aliyetumia muda wa saa 02:23:27, ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.
Katika mbio hizo zilizoanzia na kuhitimishwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo ilishuhudiwa nafasi ya kwanza hadi ya saba zikishikwa na wakimbiaji kutoka nchini Kenya huku nafasi ya nane ikienda kwa Mtanzania Paschal Mombo alietumia muda wa saa 02:30:43.
Akizungumzia siri ya ushindi wake, mbali na kusifia uratibu mzuri wa mbio hizo uliomuwezesha kukimbia bila changamoto yoyote Too alisema ni kujituma kufanya zaidi mazoezi na kukaa kambini muda mrefu ili kufanya vizuri katika michuano ya mwaka huu.
“Maandalizi ya mwaka huu ni mazuri na washiriki wameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka jambo linalotufanya wanariadha kujiwekea mikakati mizuri ili kuweza kukabiliana na ushindani mkali uliopo katika mbio hizi na ninashukuru Mungu nimefanikiwa,” alisema.
Abrahamu Too kutoka Kenya akimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye mbio za km 42 Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:22:45, akifuatiwa kwa karibu na mshiriki mwenzake kutoka nchini humo Moris Motima aliyetumia muda wa saa 02:23:19.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mbio za Rock City Marathon zilizofanyika jijini Mwanza jana ambapo alikimbia mbio za km 3 akiambatana na viongozi wengine wa serikali.
Mbali na washiriki kutoka ndani ya nchin pia pia washiriki kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo China na Marekani nao hawakuwa nyuma.
Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka akizungumza kwenye warsha ya kukabidhi zawadi kwa washindi ambapo pamoja na mambo mengine aliwapongeza waandaaji wa mbio hizo kampuni ya Capital Plus Internantional (CPI).
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mbio za Km 42 (waliosimama nyuma) mara baada ya kuwakabidhi zawadi pamoja na medali. Wengine ni pamoja na Rais wa Shirikisho la riadha nchini (RT) ambae pia ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw Anthony Mtaka(wa tatu kushoto), waandaaji pamoja na viongozi wa mchezo huo.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Bi Juliana Shonza (Kushoto) akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio za Km 42 kwa upande wa wanawake ambapo washindi wa kwanza hadi watano wote walitoka nchini Kenya.
Hivyo makala Ni Wakenya Rock City Marathon 2017
yaani makala yote Ni Wakenya Rock City Marathon 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Ni Wakenya Rock City Marathon 2017 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/ni-wakenya-rock-city-marathon-2017.html
0 Response to "Ni Wakenya Rock City Marathon 2017"
Post a Comment