NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43

NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43
kiungo : NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43

soma pia


NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43


 KAZ4


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.
Mwenyekiti wa NEC  Jaji  Semistocles  Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.
Jaji Kaijage amesema tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.
Jaji Kaijage ameainisha  kwamba kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.
Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.
“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.
Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.
Jaji Kaijage aliema Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.
Alitoa mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.
Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Zifuatazo ni Kata 43 zitazohusika katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani:
 
Na
 
MKOA
 
HALMASHAURI
 
KATA
1. ARUSHA Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Musa
Halmashauri ya Jiji la Arusha Muriet
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ambureni
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ngabobo
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Maroroni
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Leguruki
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Makiba
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Moita
2.     2

DAR ES SALAAM Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mbweni
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Kijichi
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Saranga
3. DODOMA Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Chipogolo
4. GEITA Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale Bukwimba
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

Senga
5.

IRINGA Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Kitwiru
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Kimala
6.

KILIMANJARO Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Bomambuzi
Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mnadani
Halmashauri ya Wilaya ya Hai Machame Magharibi
Halmashauri ya Wilaya ya Hai Weruweru
7. LINDI Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Chikonji
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mnacho
8.

MANYARA Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Nangwa

9.

MBEYA Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Ibighi
10.

MOROGORO Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kiloka
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Sofi
11. MTWARA Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Milongodi
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara  Mikindani Reli
Halmashauri ya Mji wa Masasi Chanikanguo

12. MWANZA Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Kijima
Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhandu
13. RUKWA Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Sumbawanga
14.  14

RUVUMA Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Lukumbule
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Kalulu
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Muongozi
15. SINGIDA Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Siuyu
16. SIMIYU Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Nyabubinza
17. SONGWE Halmashauri ya Wilaya ya Momba Ndalambo
18. TABORA Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Nata
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Muungano
19.


TANGA Halmashauri ya Mji wa Korogwe Majengo
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Lukuza
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mamba
Imetolewa leo tarehe 04 Oktoba, 2017.


Hivyo makala NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43

yaani makala yote NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/nec-yatangaza-tarehe-ya-kufanyika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NEC YATANGAZA TAREHE YA KUFANYIKA UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATA 43"

Post a Comment