title : MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA
kiungo : MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA
MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA
Na Fredy Mgunda,Mufindi
Chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimemuomba mkurugenzi kuwakopesha viwanja walimu ili kujikwamuamua na mazingira magumu wanayokumbana katika nyumba wanazoishi.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale alisema kuwa walimu wamekuwa wakiishi katika nyumba chakavu au mbali na mazingira ya shule kitu kinachosababisha kushuka kwa uwezo wa walimu kufundisha.
Kimbale alisema kuwa walimu hawana pesa za kununua moja kwa moja viwanja hivyo kwa njia ya kuwakopesha inawezekana kutokana kuwa ni waajiliwa wa serikali na mishahara yao inajulikana na ni rahisi kuresha mkopo huo.
“Sisi walimu ukitaka kujua mimi nalipwa shilingi ngapi ni rahisi tu kwa kuwa mishahara ya serikali mara nyingi inajulikana hasa pale mtumishi unapoenda kukopa mahali ndio maana tunaiomba serikali itusaidie kukopa viwanja kuwa kuwa tunauwezo wa kulipa kwa awamu tatu” alisema Kimbale
Aidha Kimbale aliwatupia lawama maafisa elimu na walimu wakuu wa shule kwa kuwanyima ruhusa bila kuwa na sababu maalum.
“Wakurugenzi amekuwa ametoa kibali upewe ruhusa lakini viongozi waliochini ya mkurugenzi wanatuwekea vipingamizi ambavyo havieleweki kitu kinachozua utata mkubwa baina ya viongozi na walimu ambao sio viongozi” alisema Kimbale.
mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamuakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Hivyo makala MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA
yaani makala yote MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/mwenyekiti-cwt-mufindi-obi-kimbale.html
0 Response to "MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE WALIMU TUNAISHI KWENYE MAPAGALE TUNAOMBA VIWANJA"
Post a Comment