title : Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo
kiungo : Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imetakiwa kusimamia weledi katika utendaji wao wa kazi na kuacha kujifanya Miungu watu kama ilivyokuwa zamani, hali iyowakatisha tamaa baadhi ya wanafunzi kuomba mikopo katika bodi hiyo.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profes Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) mpya ,amesema kuwa bodi ilikuwa inaona kero katika kuwahudumia watoto kupata mikopo na wengine walikuwa ndio sehemu ya wahitaji wa mikopo hiyo kutokana hali ya uchumi waliokuwa nao.
Amesema kuwa bodi iwaangalie watu wenye mahitaji ya kupata mikopo wapate bila kusumbuliwa katika upataji wa mikopo hiyo.Profesa Ndalichako ameitaka Bodi kusimamia vyema makusanyo ya madeni kwa wanafunzi waliosomeshwa kwa mikopo ili iweze kusaidia wengine walioomba kwa ajili ya kujiendeleza na elimu ya juu nchini kutokana na mahitaji ya waombaji ni wengi.
Amesema mpaka sasa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2014 serikali imetoa kiasi cha fedha shilingi Trilioni 3.1 huku makusanyo yakiwa Bilioni 217.Aidha amesema kulikuwa na ubadhilifu uliokuwa ukifanywa na watendaji wa bodi ya mikopo iliyopita ambayo ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alibainisha hivyo hatarajii utokee tena.
Profesa Ndalichako amesema kuwa hakuna hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kwa majina hewa, mtu anarekodiwa kuwa amechukua fedha huku akiwa marehemu lakini fedha zikiendelea kuchukuliwa hali ambayo haitajiki kujirudia.Makamu Mwenyekiti Madina Mwinyi alimuhakikishia Waziri kwamba wataweka taswira nzuri katika bodi hiyo na kuondoa changamoto zilizokuwa zikikabili hapo awali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Abdul –Razak Badru alimshukuru Waziri huyo huku akimuahidi kufanya kazi kwa kushirikiana kwa lengo la kujenga Taifa katika kuangalia vipaumbele vya mikopo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa bodi ya mikopo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya Mikopo , Madina Mwinyi akitoa maelezo jinsi bodi hiyo itavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB) Abdul –Razaq Badru akizungumza juu ya kushirikiana na bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha pamoja na bodi ya mikopo leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo
yaani makala yote Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/bodi-ya-mikopo-ya-wanafunzi-wa-elimu-ya.html
0 Response to "Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatakiwa kusimamia weledi katika utoaji mikopo"
Post a Comment