title : Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union
kiungo : Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union
Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union
Benki ya TPB imezindua rasmi promosheni ya huduma ya Western Union ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo ya kifedha kushinda fedha, simu za kisasa za mkononi na kompyuta mpakato (laptop).
Akizungumza jijini jana, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi alisema kuwa wameamua kuanzisha shindano hilo kama kuwazawadia wateja wake katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Mushi alisema kuwa washindi wanaweza kupata kiasi cha fedha ambacho kitawawezesha kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka, kulipa kodi ya nyumba na ada za watoto wao kwani watumiaji wawili wa Western Union wanaweza kushinda zawadi hadi kufikia sh Milioni 3.
Alisema kuwa mbali ya benki yao, promosheni hiyo pia itawashirikisha washirika wao kama Shirika la Posta Tanzania (TPC), Benki ya DCB, Benki ya Azania, Benki ya Wakulima ya Kagera, Benki ya Mwanga, Benki ya Amana, Benki ya Uchumi, Benki ya Maendeleo, Benki ya Njombe, Benki ya Mufindi na Benki ya Kilimanjaro.
‘’Promosheni tunayozindua leo ni ya miezi mitatu ambayo itaisha mwezi Januari 2018 na inakusudia kuwashukuru na kujiweka karibu zaidi na wateja wetu ambao wanaitumia huduma hii ya Western Union’’, alisema Frank Mushi.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi (Katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya huduma ya Western Union ambayo itawawezesha watumiaji wa huduma hiyo ya kifedha kushinda fedha, simu za kisasa za mkononi na kompyuta mpakato (laptop). Kushoto ni Kaimu Meneja wa Huduma za Fedha na Uwakala wa shirika la Posta, Rehema Mbunda na kulia ni Kolimba Tawa wa Benki ya TPB ambaye ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji
Wafanyakazi wa TPB Benki na wafanyakazi wengine wa benki hiyo na wadau kutoka Amana Benki, Azania Benki na Shirika la Posta (TPC) wakionyesha baadhi ya zawadi ambazo washindi wa promotion ya Western Union watashinda.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki ya TPB, Kolimba Tawa akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya Western Union. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi (Katikati) na Rehema Mbunda wa Shirika la Posta.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Wafanyakazi wa TPB Benki na wafanyakazi wengine wa benki hiyo na wadau kutoka Amana Benki, Azania Benki na Shirika la Posta (TPC) wakionyesha baadhi ya zawadi ambazo washindi wa promotion ya Western Union watashinda.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki ya TPB, Kolimba Tawa akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya Western Union. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Ukuaji wa Biashara wa Benki ya TPB, Frank Mushi (Katikati) na Rehema Mbunda wa Shirika la Posta.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union
yaani makala yote Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/benki-ya-tpb-kuwajaza-fedha-wateja.html
0 Response to "Benki ya TPB kuwajaza fedha wateja kupitia shindano la Western Union"
Post a Comment