title : Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali
kiungo : Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali
Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali
Mwambawahabari
Na Heri Shaban
WANAWAKE wa wilaya ya Ilala wanatarajia kupewa mikopo ya Serikali hivi karibuni ili waweze kujishughulisha na biashara ndogondo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam Jana Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema , wakati wa kuzungumza na Wanawake wa Changamka Mwanamke na Wanawake wa JUKWAA WA WILAYA ya Ilala katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Changamka Mwanamke..
"Hongereni Wanawake wa JUKWAA wa wilaya ya Ilala mmekuja kwa wingi kwa kuitikia wito
katika semina ya Changamka Mwanamke mmenifurahisha Wanawake wa wilaya ya Ilala kwa maudhurio mazuri Wanawake 700 ambao wamepata elimu katika ujasiriamali fursa nzuri Sana "alisema Mjema.
Alisema idadi hiyo ya Wanawake ambao wameshiriki kutoka Jimbo la SEGEREA, UKONGA na Jimbo la Ilala ndio watakuwa Wanawake wa kwanza kupewa mikopo ya Serikali kupitia Benki ya Dar es salaam DCB ambapo kwa sasa riba imetolewa.
Aliwataka Wanawake watakao pata mikopo hiyo watumie kwa Biashara ili wakuze mitaji yao na huku wakumbuke marejesho kwa Wanawake
watakaochukua fedha hizo.
"Wanawake wezangu sasa mjikwamue kiuchumi mikopo hii mtakayopewa muitumie vizuri elimu mliyopata Taasisi ya CHANGAMKA MWANAMKE itakuwa dira ya kuwaongoza katika biashara zenu "alisema.
Alisema atazungumza na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ili wawapunguzie bei ya mashine Za kulipia ushuru Wanawake wa Changamka Mwanamke wote nitawaita katika kikao hicho, lengo Wanawake mfanikiwe muweze kumiliki viwanda na Maghorofa.
Kwa upande wake Mwakirishi kutoka Ofisi ya Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilala Georgia Asenga alisema ILALA inategemea makusanyo ya mapato ya Halmashauri fedha shilingi milioni 508 zimeshaingia Benki,ambapo fedha zikikusanywa asilimia kumi zinaingizwa katika mikopo ili kuwagaia Wanawake na Vijana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya CHANGAMKA MWANAMKE alipongeza Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilala pamoja na msafara wake kuja katika mafunzo hayo ambayo yamewawezesha Wanawake wa Changamka Mwanamke Pamoja na Wajasiliamali wa JUKWAA wa wilaya ya Ilala kufanyiwa taratibu wa kupewa mikopo ya Serikali.
Maria alisema Changamka Mwanamke ilianzishwa 2016 inajivunia mafanikio makubwa kwa kuwa na mtandao mpana wa Wanawake wa Dar Es salaam na nje ya mkoa wa Dar es salaam na Wanawake walio ndani ya Changamka Mwanamke wote ni Wajasiliamali wana miliki miradi yao wengine changamoto mtaji watakapochukua mikopo hii itawasaidia na watarudisha marejesho kwa wakati.
Hivyo makala Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali
yaani makala yote Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/wanawake-wilaya-ya-ilala-kupewa-mikopo.html
0 Response to "Wanawake wilaya ya Ilala kupewa mikopo ya Serikali"
Post a Comment