BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE

BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE
kiungo : BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE

soma pia


BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE

Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini ​Mhe. Hussein Mohammed Bashe​ amekabidhi Vitambulisho vya Matibabu ya Bure kwa wazee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini.

Katika awamu hii ya kwanza zaidi ya wazee 1,080 watapata  Vitambulisho huku wazee 540 ndio wamekabidhiwa leo hii na wengine wataendelea kupokea kutoka katika Ofisi ya Mbunge kwa muda wa wiki nzima huku matarajio yakiwa ni kuwafikia wazee 3,284 katika jimbo zima.

Aidha, sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega ​Mhe. Godfrey Ngupula​ ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi.

​Mhe. Ngupula​ amepongeza jitihada za ​Mheshimiwa Bashe​ katika shughuli za maendeleo na kuwatumikia wananchi na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mhe. Bashe alipohojiwa alisema ya kuwa ..."wazee hawa wameitumikia nchi hii kwa muda mrefu ni jukumu letu sasa kama vijana na taifa kuhakikisha nasi tunawalipa sehemu ya nguvu kubwa walizotumia kuifikisha Tanzania hapa ilipo leo kwa kuwapatia Matibabu bora na kuwaondolea gharama za Matibabu ili kuleta unafuu wa maisha"
"Nilichokifanya ni kugharamia fedha zote za Vitambulisho ili kuhakikisha kila mzee ndani ya Jimbo la Nzega Mjini anapata kitambulisho cha matibabu ya Bure".... Hussein Bashe.

Jimbo la Nzega Mjini ni jimbo pekee ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nzega hivyo tukio hili linaifanya Halmashauri hii kuwa moja kati ya Halmashauri chache kitaifa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa Matibabu ya Bure kwa wazee.



Hivyo makala BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE

yaani makala yote BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/bashe-agawa-vitambulisho-vya-matibabu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BASHE AGAWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU KWA WAZEE JIMBONI KWAKE"

Post a Comment