Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania

Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania
kiungo : Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania

soma pia


Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania

Mwambawahabari

1
Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).Anayesikiliza  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua na Afisa Sanaa, Bona Leon Masenge.
2
Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Univerese mwaka jana, Jihan Dimachk (Kulia) na Miss Earth Tanzania, Lilian Loth.
3
Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na warembo, waandaaji na maofisa wa Basata mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja cha kujadili mashindano hayo.
……………….
Na Mwandishi wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua wakati wa kufanya tathimini ya mashindano hayo na mashindano ya urembo kwa ujumla.
Mrembo Jihan Dimachk alishinda taji la Miss Universe mwaka jana  huku Lilian Loth akishinda nafasi ya pili katika mashindano hayo.
Shalua alisema Basata wamefarijika sana na jinsi mashindano hayo yanavyoendeshwa na hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na zawadi na upendeleo.
Alisema kuwa kutokana na utaratibu mzuri wa mashindano yao, Basata imeridhia waandaaji wa mashindano hayo, kufanya mashindano ya mwaka huu na vile vile kuandaa mashindano ya kutimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2007.
“Pamoja na kuwa na shindano moja kwa kushirikisha warembo wa mikoa tofauti, bado Basata imefarijika na jinsi mnavyoendesha na utaratibu unaotumia kuwapata warembo, uendeshaji wa mashindano mpaka kumpata mshindi,”
“Tunajua kuwa kuna changamoto za wadhamini na kusababisha kufanya mashindano yenye kalenda fupi na kuondoa mlolongo wa matukio, hatua hii ni bora zaidi ili kuondoa malalamiko ya zawadi na mambo mengine, huu ni mfano wa kuigwa,” alisema Shalua.
Mkurugenzi wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajihidi kuongeza wigo ili kuona warembo wengi zaidi kutoka mikoa tofauti wanashiriki katika mashindano yao.
Maria alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini na kufikia malengo yao katika kuendeleza Sanaa hapa nchini.
“Kwa sasa kuna changamoto kubwa ya wadhamini wa mashindano, kuna haja ya kupata msaada kutoka Basata ambao ni chombo cha serikali, mnaweza kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu, tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na mamlaka ya zake kama Tanapa,” alisema Maria.


Hivyo makala Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania

yaani makala yote Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/basata-yaipongeza-kamati-ya-miss_4.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Basata Yaipongeza Kamati ya Miss Universe Tanzania"

Post a Comment