Balozi wa Morocco atembelea TADB

Balozi wa Morocco atembelea TADB - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozi wa Morocco atembelea TADB, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozi wa Morocco atembelea TADB
kiungo : Balozi wa Morocco atembelea TADB

soma pia


Balozi wa Morocco atembelea TADB



Picha ya pamoja na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mara baada ya kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB.



Na mwandishi wetu,

Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane ametembelea Ofisi za Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI alipotembelea nchini Tanzania mwezi Oktaba mwaka jana.

Mheshimiwa Benryane ambaye alifuatana na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM), ulioko nchini kwa ajili ya kikao cha pamoja cha ushirikiano na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kilimo inayotekelezwa kati ya Benki hiyo na TADB.

Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya GCAM na TADB, Mheshimiwa Benryane alisema kuwa utekelezaji wa makubaliano kati ya Mfalme wa Morocco na Rais Dkt. John Pombe Magufuli yanaendelea vizuri na kutolea mfano mashirikiano kati ya benki hizo mbili kwa upande wa miradi ya kilimo.

“Ni chini ya mwaka mmoja tangu viongozi wetu wakubaliane utekelezaji wa mikataba 21 katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kilimo, gesi, madini na na usafiri wa anga,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga aliishukuru GCAM kuichagua TADB kusimamia miradi ya utekelezaji wa makubaliano hayo kwa upande wa kilimo.

Kwa mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.

TADB imeanzishwa kwa malengo makuu ya Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.


Hivyo makala Balozi wa Morocco atembelea TADB

yaani makala yote Balozi wa Morocco atembelea TADB Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozi wa Morocco atembelea TADB mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/balozi-wa-morocco-atembelea-tadb.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozi wa Morocco atembelea TADB"

Post a Comment