title : AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI
kiungo : AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI
AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI
TIMU ya Azam FC, inatarajiwa kukipiga dhidi ya Mabatini Kombaini katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Alliance kesho Jumatano kuanzia Saa 10.00 jioni.
Kikosi cha Azam FC kipo hapa mkoani Mwanza tokea juzi, kikifanya maandalizi ya kuikabili Mbao, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unaotarajiwa kufanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu uliopita wanaodhaminiwa na Maji Safi ya Uhai Drinking Water, Benki Bora ya NMB na Tradegents, wanatarajia kuutumia mchezo huo wa kirafiki kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wao na Mbao.
Hadi hivi wachezaji wote wa Azam FC wako fiti, isipokuwa kipa Razak Abalora, anayesumbuliwa na Malaria, ambaye leo ameanza mazoezi mapesi wakati kikosi hicho kilipofanya mazoezi ya asubuhi katika Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa Mwanza.
Kueleka mchezo wa Mbao, Azam FC imeonekana kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni miongoni mwa timu nne zilizokaa kileleni zote zikiwa na pointi 12, zingine zilizojuu yake zikiwa ni Simba, Yanga na Mtibwa Sugar, ambazo ziko juu yake kwa idadi ya mabao ya kufunga.
Hivyo makala AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI
yaani makala yote AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/azam-fc-kucheza-mechi-ya-kirafiki-na.html
0 Response to "AZAM FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MABATINI KOMBAINI KESHO JIONI"
Post a Comment