title : YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC.
kiungo : YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC.
YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC.
MwambawahabariYanga ina uhakika itaifikia Simba leo kwa pointi kama itaibuka na ushindi katika mechi yake dhidi ya Njombe FC.
Pamoja na kwamba Yanga iko ugenini, ina nafasi hiyo kama itapata pointi tatu kwa kuwa tayari ina moja baada ya kuanza na sare dhidi ya Lipuli FC.
Simba iliyoanza kwa kishindo cha mabao 7-0 dhidi ya Lipuli FC, jana ilikwama dhidi ya Azam FC baada ya kupata sare ya 0-0 ikiwa ugenini Chamazi.
Kama Yanga itashinda na kufikisha pointi 4 kama ilivyo kwa Simba, maana yake rasmi vita ya ubingwa itakuwa imeanza kwa kila upande na itachangia ligi hiyo kuamka.
Simba itakuwa inajivunia akaunti nzuri ya mabao lakini itakuwa na hofu katika pointi. Hivyo mashabiki wengi wa Simba watakuwa wakiomba Yanga ipoteze ili kutengeneza ahueni kwao.
Hata hivyo, Yanga wanalazimika kufanya kazi ya ziada kwa kuwa Njombe iliyopanda daraja inaonekana imejipanga kufanya vema.
Mechi hiyo mjini Njombe ndiyo itakayotupiwa macho na watu wengi zaidi ili kujua Yanga inaifikia Simba na kuanza mbio za kutetea ubingwa wake.
Hivyo makala YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC.
yaani makala yote YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/yanga-kukipiga-leo-na-njombe-fc.html
0 Response to "YANGA KUKIPIGA LEO NA NJOMBE FC."
Post a Comment