title : Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo
kiungo : Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo
Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo
Na Khadija Khamis – Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Issa Haji Gavu amewataka Watumishi Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni kuitumia vizuri fursa ya mafunzo walioipata ili kuzidisha ufanisi katika kazi zao .
Alisema ikiwa wataitumia vyema vizuri fursa hii katika kujipatia mafunzo ya upishi na ukarimu wataongeza utaalamu na kuweza kupata mbinu zaidi ya kubadilishana uzoefu kwa namna moja au nyengine .
Hayo aliyasema katika ufunguzi wa mafunzo ya wiki moja ya watumishi wahudumu wa Viongozi wa Serikali uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Kikwajuni yatayoendeshwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China (China National research Institute of food and Fermation Industries).
Aidha alisema mafunzo hayo yatarahisisha kutafsiri nadharia halisi zitazofundishwa na kuona uhalisia wa mambo yanavyokuwa pamoja na kubadilishana uzoefu na kuzidisha ushirikiano .
Aliwataka washiriki kuwa makini katika kuzingatia muda wote wa masomo pamoja na kutoa mashirikiano kwa wakufunzi ili waweze kuwa na ari ya ufundishaji pia wasisite kuuliza maswali iwapo watakuwa hawajafahamu, ili lengo la mafunzo hayo yafanikiwe.
“Wengi wenu bado mna umuhimu wa kutafuta elimu hasa mkizingatia kwamba elimu haina mwisho na ndio dira ya mafanikio katika kulipeleka mbele Taifa hasa katika wakati huu wa sayansi na teknolojia.” alisema Waziri.
Alifahamisha jinsi ya makubaliano ambayo yaliofikiwa na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuwapatia mafunzo watendaji wake ya upishi na ukarimu iwe chachu ya kujipatia maendeleo kwa jamii .
“Faraja urafiki na uhusiano uliodumu kwa muda mrefu uendelee kudumu baina ya Ndugu zetu hao wa Serikali hizo, “alisema Waziri Gavu .
Hata hivyo alitoa rai kwa wakufunzi hao kuweza kujifunza mambo mbali mbali ya kihistoria hapa Zanzibar na kutembelea sehemu za kivutio pamoja na kuona miti ambayo ni maarufu kwa viungo ambavyo vinatumika Zanzibar .
Nae Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China Xie Xiaowi alisema wataendelea kudumisha mashirikiano baina yao pamoja na udugu wao ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni katika nchi hizo .
Nae mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mvita Khamis alisema amefurahishwa kupata fursa hiyo ya mafunzo ya mapishi na ukarimu anatarajia akimaliza atayatumia ipasavyo kwa uweledi mkubwa katika kutoa huduma bora kwa Viongozi na wageni .
Hivyo makala Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo
yaani makala yote Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/watumishi-na-wahudumu-wa-viongozi-wa.html
0 Response to "Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo"
Post a Comment