Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu

Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu
kiungo : Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu

soma pia


Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu

Mara baada ya kikao cha kwanza kwenye mkutano wa 8, wa Bunge la 11, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesema wale waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi, sasa wataona dhahiri udhaifu wake uko wapi.

Spika Ndugai ameeleza hayo wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Taratibu zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu, nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako maneno kama haya hayana umuhimu”, alisema Spika Ndugai.

Sambamba na hilo, Spika Ndugai amewakaribisha wabunge walioapishwa huku akiwafunda wabunge wengine, kwamba kiapo walichokula wenzao leo kiwakumbushe utii na uaminifu kwa kwa tiba ya nchi.

“Kiapo hiki cha uaminifu kina tukumbusha wengine ambao tuliapa utii wa Katiba na kiapo chetu kwa ujumla wake, kuhusiana na uaminifu na utii.  Ni vizuri kuisoma Katiba na kuipitia ili uweze kujua nafasi ya vyama vya siasa na uhusiano wa mbunge na chama cha siasa”, alisisitiza Spika Ndugai.

Wabunge hao ambao wameapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati na kuanza kazi mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.


Hivyo makala Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu

yaani makala yote Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/09/spika-ndugai-atuma-salamu-kwa-wabunge.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Spika Ndugai Atuma Salamu kwa Wabunge Waliodai Yeye ni Dhaifu"

Post a Comment